Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw.
Servacius Likwalile (kushoto) akikisaini Mkataba wa mkopo wenye masharti
nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha
kituo cha utafiti wa magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha
Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam.
Kulia ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero akisaini
mkataba huo kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt. Donald Kaberuka.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando (kushoto) akitoa neno la shukurani
baada ya kusainiwa Mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki
ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa
magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo jijini Dar es salaam. Wa kwanza kulia
ni Muwakilishi wa Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero na katikati ni
Katibu Mkuu Wizara ya fedha Bw. Servacius Likwalile.
………………………………………………………………
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali ya Tanzania imetiliana
saini mkataba wa mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya Dola za
Kimarekani milioni 9.4 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 15.5 kutoka Benki
ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kuboresha kituo cha utafiti wa
magonjwa ya moyo kinachosimamiwa na Chuo Kuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Mkataba huo wa makubaliano
umesainiwa leo jijini Dara es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Muwakilishi wa
Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero kwa niaba ya Rais wa benki hiyo Dkt.
Donald Kaberuka.
Dkt. Likwelile alisema kuwa kituo
hicho kitasaidia kupunguza tatizo la wataalam wa afya nchini na nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na hivyo kupunguza idadi kubwa ya
wagonjwa wanaotibiwa nje ya nchi.
Kwa upande wake Muwakilishi wa
Benki ya ADB nchini Tonia Kandiero ameipongeza Tanzania kuwa nchi ya
kwanza kusaini mkataba huo kati ya nchi nne za jumuiya ya EAC
zinazokusudiwa kujenga kituo kama hicho.
Bi Tonia alisema kuwa benki ya ADB
imejiwekea lengo kuboresha rasilimali watu katika fani ya afya ambapo
mradi wa ujenzi wa kituo kinachojengwa MUHAS upo katika mkakati wa benki
hiyo ambao uulianza 2011 hadi 2015, mpango mkakati wa benki wa 2013
hadi 2017 na mfumo mpya wa elimu katka nchi za Afrika.
Mfumo huo unalenga kutatua tatizo
la utaalaam katika soko la ajira kwa kupitia vituo bora vya kanda vya
afya ili kuendana na dira ya maendeleo ya Taifa na mkakati wa kupunguza
umasikini ifikapo mwaka 2025.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mbando ameushukuru uongozi wa
benki ya ADB kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuahidi fedha
hizo zitatumiwa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Hadi kukamilika kwa kituo hicho
cha afya kinachojengwa katika chuo cha MUHAS kitagharimiwa na benki ya
ADB kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment