kurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam. |
Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, Matha Samwel akizungumza na vyombo vya habari katika uzinduzi wa ripoti ya Kutokomeza Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE) leo jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka akizungumza na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa waliokuwa katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam. |
Baadhi ya wanahabari na viongozi wa vituo vya taarifa na maarifa wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa ripoti ya GEWE jijini Dar es Salaam Makao Makuu ya Ofisi za TAMWA Sinza Mori Dar es Salaam. |
Akizinduwa ripoti hiyo leo jijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake
Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka alisema mradi huo umekuwa na
mafanikio makubwa kwa jamii katika kujitambua na kuibua vitendo vya
Ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari kuibua vitendo
hivyo zaidi ya hapo awali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Bi. Valerie Msoka pamoja na meza kuu wakionesha ripoti ya GEWE mara baada ya uzinduzi wake leo jijini Dar es Salaam. |
CHAMA cha Wanahabari Wanawake
Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na taasisi anuai za kijamii
kimezinduwa tathmini ya ripoti juu ya utekelezaji wa mradi wa Kutokomeza
Ukatili na vitendo vya Unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto (GEWE).
Alisema idadi kubwa ya habari,
makala na vipindi vya redio na televisheni juu ya masuala ya ukatili
vimefanywa maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo limeonesha mafanikio
ikiwa ni pamoja na jamii kuelewa zaidi masuala ya ukatili na unyanyasaji
na wengine kuanza kuyapiga vita kwa ushirikiano.
Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa
TAMWA alisema mradi huo ulitekelezwa kwa pamoja kwa ushirikiano wa
Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Chama cha Wanasheria Wanawake
Tanzania (TAWLA), Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na
Kituo cha Usuluhishi cha TAMWA (CRC), kinatekeleza mpango wa kutokomeza
ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (GEWE II)
katika wilaya 10 za Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa upande wake Matha Samwel
Mratibu wa Mradi wa GEWE kutoka TGNP Mtandao, akizungumza alisema mradi
huo umekuwa na mafanikio makubwa kiasi cha kuibua changamoto ambazo
zinaitaji utatuzi kwa ushirikiano na wadau wengine mbalimbali.
“…Katika kipindi cha utekelezaji
wa mradi wa GEWE kumekuwa na mafanikio makubwa, moja wapo kubwa ni
kuanzishwa kwa vituo vya taarifa na maarifa katika wilaya zote 10 za
mradi, ambapo vituo hivyo vimekuwa vikitumika kama sehemu ya kutolea
taarifa kwa jamii…sehemu ambayo wanajamii wanawake na wanaume wanakutana
na kubadilishana taarifa na kuangalia namna ya kutatua matatizo yao
yanayotoka katika jamii kama kubakwa, vipigo au kulawitiwa na
mengineyo,” alisema Bi. Samwel.
Hata hivyo aliongeza kuwa vituo
vya taarifa na maarifa vimekuwa na msaada mkubwa katika maeneo hayo
kwani jamii zimeweza kuvitumia pia kwa kujadili namna ya kukuza uchumi
kwenye familia zao kwa kuanzisha vikundi vya kijasiriamali
vinavyochangia pia kupunguza umasikini kwenye jamii suala ambalo
linachangia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.
Anasema vituo vya taarifa na
maarifa vimekuwa vikiunganisha nguvu na serikali na vyombo vingine vya
dola kuhakikisha wanapambana na vitendo vya ukatili kwa kuhakikisha
sheria inachukua mkondo wake kwa watu wanaohusika ama kutuhumiwa na
vitendo vya ukatili. Alitolea mfano katika eneo la Mwananyamala Kituo
cha Taarifa na Maarifa kilishirikiana na Serikali kwa kuibua taarifa ya
kuteswa kwa binti wa kazi za ndani na mwajiri wake jambo ambalo
liliwezesha bosi huyo kufikishwa mahakamani.
“…Hivyo waweza kuona matokeo
makubwa katika mradi wa GEWE ni kuanzishwa vituo vya taarifa na maarifa
sehemu ambayo imekuwa ni kimbilio la wengi, na pili ni nguvu ya pamoja
ya jamii katika uwajibikaji. Lakini changamoto iliyopo sasa ni namna ya
kuwasaidia kwa kuwaifadhi waathiriwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia
katika jamii,” alisema Mratibu huyo.
Aidha aliitaka Serikali na wadau
wengine kujitokeza na kushirikiana katika kujenga kituo kikubwa cha
kuwasaidi wananchi ambao wamekumbana na ukatili wa kijinsia wakati
wakipatiwa huduma kabla ya kurejea katika jamii yao. “…Mfano kumekuwa
kuna mabinti hata hapa Dar es Salaam wamekuwa wakikimbia kukeketwa na
familia zao lakini hakuna sehemu ya kuwaifadhi, hivyo tunaiomba Serikali
na wadau wengine wajitokeze ili kuunganisha nguvu tujenge kituo hiki,”
alisema.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment