Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa
ufafanuzi kuhusu ushiriki wa Wanajeshi katika uboreshaji wa zoezi la
uandikishaji wa daftari la kupiga kura.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
Tume inasema kutakuwepo na wanajeshi 6 wa Jeshi la Wananchi ambao kazi
yao ni kusaidia shughuli za lojistiki kama vile kuhamisha vifaa kutoka
kata moja kwenda nyingine.
Pia wanajeshi hao watasaidia
katika shughuli za kufanya matengenezo madogo madogo ya vifaa yanayoweza
kujitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji.
Taarifa inasisitiza kuwa
Wanajeshi hao hawatakuwepo kwenye vituo vya uboreshaji wala hawatahusika
na zoezi la uandikishaji kama baadhi ya vyombo vya habari
vilivyoripoiti hivi karibuni.
Aidha katika mkutano na Vyama
vya Siasa uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam ulifafanua kuwa
watendaji watakaohusika katika zoezi hilo ni maafisa waandikishaji na
wasaidizi wao, waandishi wasaidizi, wataalamu wa fani ya TEHAMA na
wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
No comments:
Post a Comment