Wachezaji wa timu ya COSS (College
of Social Science) ya chuo kikuu cha Dar es salaam kwenye picha ya
pamoja wakati wa kujiandaa kucheza. Kikosi hiki ndicho kinachoongoza
kundi B la wanaoshindana chuoni hapo.
……………………………………………………………………………………
* SJMC (School of Journalism & Mass communication) wanaongoza kilele cha group A
* COSS (College of Social Science) wanaongoza kilele cha group B
* Mechi zingine nne kuendelea leo hadi Jumamosi
* COSS (College of Social Science) wanaongoza kilele cha group B
* Mechi zingine nne kuendelea leo hadi Jumamosi
Mashindano ya mpira wa miguu kwa
wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yanayojulikana kama
Airtel UNI255 yanayoshirikisha wanafunzi wote wa schools na Colleges
zilizopo chuoni hapo yameendelea kwa kasi yakiwa leo yameingia siku ya
tatu toka kuanza kwake huku baadhi ya washiriki wakijichukulia ushindi
na kuongozo msimamo wa mchezo huo na wengine kuendelea kusuasua .
Akiongea kuhusiana na mwenendo wa
mashindano hayo kwa sasa Waziri wa michezo wa jumuiya ya wanafunzi chuo
kikuu cha Dar es salaam STANLRY JULIUS alisema “Mashindano ya mwaka huu
yamekuwa na mvuto wa kipekee hasa kutokana na wadhamini wetu Airtel
kutupatia vifaa vya kutosha na kwa namna moja yameongeza hari sana kwa
washiriki wote
Hadi sasa kinara wa kundi A ambao
mechi zao zinachezwa pale katika viwanja vya ndani chuo kikuu cha Dar
es salaa ni SJMC (School of Journalism and Mass Communication) alicheza
mechi mbili na kushinda zote na kujitengenezea pointi 6 na huku
akiongoza kwa kuwa na bao 5 za kufunga.
Kundi B ambao mechi zao
zinazochezewa katika viwanja vya chuo kikuu za Mabibo maarufu kama
Mabibo Hostel linaongozwa na COSS (College of Social Science) ambapo
imecheza mechi 3 ikashinda moja na kutoa sare ya bila kungana mechi 2.
Kwa matokeo hayo wanapointi 5 na goli 2.
Mashindano haya ya Airtel UNI255
yanaendelea tena leo na yatafikia tamati siku ya jumamosi kwa fainali
itakayokutanisha mshindi wa kundi A na kundi B na baadae Airtel imeandaa
tamasha maalum la vipaji maalum kwa wanafunzi wa chuo hicho
litakalofuatiwa burudani kali toka kwa wasanii maarufu wa kizazi kipya
nchini akiwemo shilole, Ney wa Mitego, Roma na wengineo. Aidha katika
kilele cha tamasha hilo Airtel itazindua kwa wanafunzi wa chuo kikuu
huduma ya UNI255 itakayowawezesha kuwasiliana , kuperuzi internet kwa
gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment