Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Songea, Dk Emmanuel
Nchimbi anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismasi Wilayani
Singea mkoani Ruvuma linalotarajia kufanyika Desemba 28 kwenye uwanja wa
Majimaji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama Nchimbi
amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo ambalo lengo lake ni
kufikisha ujumbe wa neno la Mungu kwa jamii.
“Nchimbi amekubali kuwa mgeni rasmi katika tamasha la Krismasi
mkoani Ruvuma, hivyo wadau wa muziki wa Injili wajiapange vilivyo kwa
lengo la kupata uinjilishaji, utakaofanywa na maaskofu na waimbaji,”
alisema Msama.
Msama alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Desemba 25 kwenye
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na Desemba 26 litafanyika kwenye uwanja
wa Samora mkoani Iringa.
Msama alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
kujitokeza kwa wingi kwani tamasha hilo lina lengo la kufanikisha
matakwa ya wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane.
No comments:
Post a Comment