Na Mahmoud Ahmad Arusha
WILAYA ya Temeke Mkoani Dar es
Salaam inaongoza kwa matukio ya watoto kufanyiwa ukatili wa kijinsia
kwa matukio 45 sawa na asilimia 4 huku Mkoa wa Kagera ukifuatia kwa
matukio 36 sawa na asilimia 3.
Aidha Mkoa wa Arusha matukio yanayoongoza ni 36 kati ya
hayo matukio makubwa ni ya watoto yanayotokana na unyanyasaji wa
vipigo majumbani unaofanywa na wazazi/walezi wa watoto hao.
Hayo yalisemwa jana na Michael
Kihongo kutoka Shirika la Ustawishi na Utetezi wa Haki za
Watoto(SISEMA), wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii
juu ya kampeni ya kampeni ya Huduma ya Simu kwa Mtoto ijulikanayo kwa
jina la kingereza Care For Me! Quality Care for Every Child inayokwenda
sambamba na upigaji wa simu ya bure kupitia
namba 116 na kutoa habari za unyanyasaji wa watoto unaofanyika mahali popote.
Alisema tangu kampeni hiyo
ilpozinduliwa mwaka jana hadi leo hii Wialaya ya Temeke inaongoza kwa
matukio ya watoto kunyanyaswa na kwamujibu wa matukio ya nchi nzima
ambayo yameripotiwa tangu kampeni hiyo ilipoanza hadi leo hii matukio ya
unyanyasaji wa kijinsia ni 139 sawa na asilimia 6 huku matukio ya
kutelekezwa kwa watoto yakiwa ni 91 sawa na asilimia 4.
Pia matukio ya utumikishwaji wa watoto ni 70 huku matukio ya watoto kutukutunzwa na wazazi/walezi wao ni 62 ubakaji 28.
“Tangu kampeni hiyo ilipoanza
hadi leo hii matukio ya watoto yameripotiwa kuwa mengi na walipokea
jumla ya simu 27,545 huku simu 2,362 zikiwa ni simu zenye uhitaji wa
kushughulikia na zilizobaki ni za kutekelezwa.
Naye Mratibu wa Utetezi wa Shirika laSOS Bara na Visiwani,
John Baptista wakati alipokuwa akizungumzia kampeni ya Huduma ya Simu
kwa Mtoto lijulikanalo kwa jina la kingereza Care For Me! Quality Care
for Every Child inayokwenda sambamba na upigaji wa simu ya bure kupitia
namba 116 na kutoa habari za unyanyasaji wa watoto unaofanyika mahali
popote.
Pia alisema vituo zaidi ya 180 nchi nzima ndio zinalea watoto
wanaoishikwenye mazingira hatarishi kati ya hivyo 39 tu ndio
vimesajiliwa huku kwa Mkoa wa Arusha vituo vinavyofanya kazi ni 13 huku
vingine vikitoa huduma kwa watoto bila kusajiliwa pia akaitaka idara ya
maendeleo ya jamii kufanyakazi kwa ukaribu na kuweza kuibua tafiti
mbalimbali zitakazo weza kuondokana na tatizo hili.
Alitoa rai kwa serikali kutenga
bajeti zaidi kwaajili ya mahitaji ya watoto pia alitoa rai kwa wadau
mbalimbali kushirikiana kwa pamoja ili kuwasaidia watoto wanaoishi
kwenye mazingira hatarishi waweze kuishi maisha sawa na wakiwa na
familia zao.
No comments:
Post a Comment