Mahmoud Ahmad Arusha
Mjadala wa akaunti ya Tegeta
Ascrow hauna tija katika kampeni za uchaguzi wa serikali za na ulifungwa
Bungeni na Serikali ipo mbioni kuwachukulia hatua wale wote
watakaobainika kuhusika na upotevu wa fedha hizo hivyo sio muda sahihi
wa kuunadi kwa wananchi katika mikutano ya hadhara bali vyama vya siasa
vinatakiwa kunadi sera vitawafanyia nini wananchi wakivipa ridhaa.
Kauli hiyo imetolewa jana na
Katibu wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Arusha, Feruzy Banno ,wakati
akiwanadi wagombea wa chama cha Mapinduzi katika kata za Unga Ltd na
Daraja Mbili huku akiwata wanachi kuwachaguwa wagombea wa CCM.
Banno, amesema kuwa mjadala wa
Ascrow kwa sasa ulishafungwa bungeni na wagombea wa vyama mbali mbali
katika uchaguzi wa sarikali za mitaa wanatakiwa kunadi sera badala ya
kuweka mjadala huo katika kampeni kwani sarikali ipo teyari kuyafanyi
kazi maazimio ya bunge.
Alisema kuwa CCM imejipanga
katika kunadi sera za kuwaondolea wananchi kero mbali mbali
zinazowakabili na kuwaambia wananchi CCM katika kipindi cha miaka mitano
wametekeleza kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.
“ Ifike pahali vyama vya siasa
vinanadi Sera badala ya kuendeleza siasa chafu za Matusi na Kejeli kwa
wagombea wananchi wanataka kuona wagombea watawafanyia nini iwapo
watawapatia ridhaa na kamwe wananchi hawahitaji matusi na kejeli
‘alisema, Banno.
Amesema ukiona vyama vinatumia
matusi na kejeli kwenye kampeni zake badala ya kuwaeleza wananchi
watawafanyia nini mtambue kuwa vyama hivyo vimefilisik kisiasa kwa kuwa
havina cha kuwafanyia wananchi .
Nae Mgombea wa CCM Mary Thomas
akiomba kura aliwataka wakazi wa Mtaa wa Tindiga kata ya Unga
limited,kumpa ridhaa ili kumwezesha kushirikiana katika kuharakisha
maendeleo na huduma zingine za kijamii ikiwemo kutatua kero mbali mbali
zinazoukabili mtaa huo.
Kuhusu gharama za ulinzi na
usafi ambazo zinachangiwa na wananchi ,Mary, amewaambia wananchi kwamba
haiwezekani shughuli za ulinzi na usafi kufanyika bila ya kuchangiwa
fedha kwa ajili ya huduma hiyo,hivyo akaomba wananchi kuwahoji hao
wanaodai kuwa shughuli hizo zitafanywa bure, nani yuko tayari kufanya
shughuli hizo bila ya kupokea ujira.
Amewaambia wananch kuwa
atawaambia ukweli na kamwe hayuko tayari kueleza uongo ili achaguliwe la
hasha, kwa kuwa anatambua changamoto zilizopo katika shughuli za ulinzi
na usafi hivyo lazima zichangiwe ili ziweze kufanyika
Kwa upande wake mgombea unyekiti
wa Mtaa wa Darajani Mahmoud Said ,alisema kuwa wanaopanda kwenye
majukwaa na kuwaambia wananchi kuwa wataondoa malipo hayo ya huduma za
ulinzi na usafi wameishiwa sera na hawapo kwa ajili ya kuhamasisha
maendeleo katika mtaa huo.
Amewaambia wananchi kuwa
haiwezekani shughuli za usafi na ulinzi wa mtaa zifanyike bila ya
kuchangiwa kwa kuwa wanaozifanya nao wanamahitaji .
Alisema kuwa akipewa ridhaa ya
kuchaguliwa katika nafasi hiyo atatekeleza kwa vitendo ilani ya CCM na
kuwa ana mipango endelevu kwa vijana wa mtaa huo katika kukabiliana na
suala zima la ajira kwa vijana.
No comments:
Post a Comment