TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Wednesday, December 10, 2014

TRA KUCHAMBUA RIPOTI YA KITUO CHA UTAFITI CHA KODI CHA KIMATAIFA (ICTD)

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo, Prof Mick Moore, wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
 Wataalamu wa kimataifa
wa masuala ya kodi  wakiendesha
mjadala katika mkutano wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala
ya kodi,mkutano uliofanyika jana  jijini Arusha ,Kamishna Msaidizi wa Mamlaka
ya Mapato Uganda (URA), Milly Nalukwago (kushoto),
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade (katikati) na  Mtaalam wa Kodi wa Uingereza, Rhiannon Mc Cluskey.
Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA RISHED BADE
kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Prof MICK MOORE wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
Mwakilishi  wa Channel Ten Arusha, Jamila Omar (katikati) , Mwakilishi wa kituo cha Star TV Arusha, Ramadhani Mvungi ,Iddy Uwesu wa Azam tv Arusha wakifanya mahojiano maalumu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)  Rished Bade jijini Arusha wakati wa
mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo.
 ***********
maendeo mbalimbali nchini.Mamlaka ya mapato nchini TRA imeanza kuchambua ripoti
ya utafiti uliofanywa na kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi na maendeleo
inayobainisha changamoto mbalimbali za ulipaji kodi katika
Zoezi la uchambuzi wa ripoti hizo linatajwa kuwa na shabaha ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuboresha mifumo ya sheria na ulipaji kodi kwa hiari.
Sehemu ya Taarifa ya utafiti uliofanwa katika kipindi cha mwaka uliopita na kituo cha kimataifa cha kodi na  maendeleo katika mikoa mbalimbali nchini, inabainisha mazingira tofauti ya ulipaji wa kodi ambapo baaadhi ya maeneo yameonekana kuwa katika changamoto kubwa za ukwepaji kodi.
Kamishana wa TRA Rished Bade kizungumza Jijini Arusha wakati wa Mkutano wa kimataifa baina yao na kundi la wataalamu, wanaofanya utafiti kuhusu masuala ya kodi duniani amesema pamoja na mapitio ya ripoti za utafiti wa taasisi hiyo,fursa hiyo inatoa mwanya kwa wataalamu wa ndani kujifunza mbinu za kushughulikia changamoto za walipa kodi wanaofanya biashara za kimataifa.
Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Profesa
Mick Moore ameeleza kusudio la tafiti zao katika nchi mbalimbali za Afrika kuwa
unalenga kuimarisha mifumo ya kodi hususani katika sekta za maliasili zikiwemo
Madini,Gas na Mafuta.
Katika hatua nyingine Mamlaka ya mapato nchini TRA imeibuka kinara kwa kuwa na hesabu bora miongoni mwa taasisi za serikali kwa mwaka 2013-2014 zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini NBAA ambapo kamishna wa mamlaka hiyo akizungumza Jijini hapa katika hafla ya kukabidhiwa ushindi huo amesema hatua hiyo inazidi kuwajengea imani walipa kodi juu ya utendaji wa chombo hicho.
Raha tele tabu ya nini?: zinaonyesha ongezeko la idadi ya walipa kodi chini,idadi iliyopo sasa inatajwa kuwa ndogo kulinganisha na mataifa mengine kutokana na mfumo wa kibiashara usio rasmi unaopelekea kupunguza idadi ya walipa kodi wanaofikia milioni moja nukta  nane hivi sasa.
============================================================

“MSICHANGIE SHEREHE PEKEE CHANGIENI NA MATIBABU”-DC SIKONGE

Mkuu wa wilaya ya Sikonge Bi.Hanifa Selengu akimkabidhi kadi ya kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii  CHF mmoja kati ya wakulima wa tumbaku katika kijiji cha Kisanga wilayani humo wakati wa kampeni ya Uzinduzi wa mfuko huo. 
Mkuu wa wilaya ya Sikonge akikabidhi kadi ya CHF kwa mkazi wa kijiji cha Kisanga wilayani humo
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kisanga waliohudhuria uzinduzi wa kampeni hiyo ya uhamasishaji kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF wilayani Sikonge.
Wananchi  wakiwa wamekaa  chini ya mti wa Mwembe wakisiliza kwa makini maelezo kuhusu faida za kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF,wakati wa uhamasishaji mfuko huo.
Meneja wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kanda ya Magharibi Bw.Emmanuel Adina akigawa vipeperushi kwa wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF katika kijiji cha Kisanga.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima Afya NHIF kanda ya Magharibi Bw.Emmanuel Adina akitoa ufafanuzi kuhusu kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii.
 JAMII imeshauri kubadilika na kujenga tabia ya kuchangia matibabu kupitia mifuko ya (NIHF) na (CHF) na kuachana na tabia ya kupenda kuchangia sherehe pekee badala yake wajitoe kuchangia na matibabu.
Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NIHF) kanda ya magharibi Emmanuel Adina alisema hayo wakati akiongea na wananchi wa kata ya Kisanga wilaya ya Sikonge mkoani Tabora siku ya uzinduzi wa mfuko wa afya ya jamii (CHF).
Adina alisema jamii imejenga tabia ya kupenda kuchangia harusi na sherehe nyinginezo tena kwa kiwango kikubwa lakini linapokuja suala la kuchangia mifuko ya afya kwa ajili ya kupata matibabu bora jambo hilo linakuwa zito.
Alisema kiwango cha uchangiaji kwa wilaya ya Sikonge ni sh 5,000 na matibabu yatapatikana kwa muda wa miezi 12 kwa mume,mke na watoto nane.
Adina alisema afya ni jambo muhimu duniani na kama taifa lolote halina jamii yenye afya bora basi taifa hilo katika kuzalisha mali na kukuza uchumi ni ndoto.
Alibainisha mfuko wa afya ya jamii CHF ni mkombozi wa wananchi ambao wako kwenye sekta binafsi hivyo ni vyema jamii ikahamasika kujiunga nao.
Meneja huyo katika hatua nyingine alichangia kaya tano ambazo hawana uwezo na wako kwenye mazingira magumu ya kimaisha.
Aidha meneja huyo alifanikisha kupata wanachama wapya katika kata hiyo ikiwa ni jumla ya kaya 614 huku kaya wengine wakihamasika kujiunga na mfuko.
Adina aliwashawishi wananchi hao kutumia fursa walizonazo ikiwemo tumbaku kilo mbili tu zinatosha kujiunga na mfuko baada ya mauzo,jogoo na biashara ndogo walizonazo kwani matibabu ni jambo zuri kwa afya zao na kwamba ugonjwa unapokuja hautoi taarifa.
Aidha alibainisha kuwa mwananchi yoyote ambaye atashawishi mwanachama kujiunga na mfuko wa CHF atapewa kiasi cha sh 500 kama motisha ya kusababisha mfuko kupata mwanachama mpya.
==============================================================

DAR LIVE YAFURIKA KATIKA KILELE CHA EFM BAR KWA BAR MUZIKI MNENE

Inspector Haroun ‘Babu’ akifanya makamuzi wakati wa kilele cha EFM Bar kwa Bar Muziki Mnene ndani ya Dar Lve jana.
Nyomi iliyohudhuria sherehe za kilele hicho.
Burudani mwanzo mwisho.
DJ mkongwe nchini, Majay Majizzo akifanya yake stejini na kupagawisha mashabiki vilivyo.
Babu aliamua kuvua viatu na kubaki peku baada ya burudani kukolea.
Ma DJ kutoka EFM wakitoa burudani.
Mtangazaji wa Michezo wa EFM Radio, Maulid Kitenge akiwaburudisha mashabiki.
Wafanyakazi wa EFM Radio wakiwa katika pozi wakati wa kilele cha EFM Bar kwa Bar Muziki Mnene.
Kitenge katika pozi na mdau.
Mtangazaji wa EFM, Ssebo katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiano wa EFM, Kanky Mwaigomole.
Watangazaji na Ma DJ wa EFM wakifanya yao ndani ya Dar Live.
UMATI wa wapenzi wa burudani jana ulifurika katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala, Zakheem jijini Dar katika kilele cha matamasha yaliyoandaliwa na EFM Radio yajulikanayo kama Bar kwa Bar Muziki Mnene.
Burudani kutoka kwa Inspector Haroun zilikonga vilivyo nyonyo za mashabiki huku DJ Makey, watangazaji wa EFM Maulid Kitenge na mwenzake Omary Katanga wakiwapa raha tosha mashabiki waliofurika katika ukumbi huo.
(PICHA NA PATRICK BUZOHELA / GPL)
==================================================================

Coastal Union wazuru kaburi la marehemu Zakaria Kinanda

unnamed Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji,Salima Bawaziri akiwaongoza wanachama na wapenzi wa timu hiyo kupiga dua kwenye kaburi la marehemu Zakaria Kinanda juzi Kabla ya timu ya Coastal Union U-20 kucheza mechi ya Kirafiki na timu ya Monga Stars ambapo Coastal Union U-20 ilishinda bao 1-0,Picha kwa hisani ya Coastal Union
==============================================================

Nyalandu: Hatuna mpango kufukuza Wamasai Loliondo

unnamed8
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akijaribu kurusha mkuki alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
unnamed
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiagana na mzee wa kimasai mara baada ya kumaliza mkutano uliokuwa na lengo la kukanusha uvumi juu ya kuondolewa kwa jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
unnamed1
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael Rong’oi akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (aliyekaa kwenye pikipiki).
unnamed2
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanawake wa jamii ya kimasai mara baada ya kumaliza mkutano nao.
unnamed4
Wamasai wakichukua kumbukumbu muhimu katika mkutano wao na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
unnamed5
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na Wamasai waliokusanyika kwa ajili ya kusikia tamko la serikali juu ya uvumi wa kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
unnamed6
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akionja maji kutoka katika kisima kilichojengwa kwa ajili ya kutatua tatizo la maji katika katika eneo la Loliondo.
………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu, amesema habari zinazodai kuwa Serikali inataka kuwaondoa wakazi wa zaidi ya 40,000 katika eneo la Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha hazina ukweli wowote.
Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.
Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.
Akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.
“Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.
========================================================================

Hazina yapamba tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne

unnamed6Waamuzi ambao ni Wahadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt.Kedmon Mapana (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Delphine Njewele (wa kwanza kulia) wakionesha utaalamu wao wa sanaa kwa kusakata mzuki kwa saili ya “Kwaito” wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
unnamed5Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Serikalini (GCU) Ingiahedi Mduma (katikati) wakati wakitoa burudani wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es unnamed4Meneja Mawasiliano Jamii kutoka Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania (MCA-T) Margaret Mussai akifafanua jambo kwa mteja wake Mashaka Kindamba mkazi wa Mtoni Mtongani Wilayani Temeke wakati alipotembelea banda hilo wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
unnamed3Mwamuzi wa michezo ya sanaa za maonesho na Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Stephen Ndibalema (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkaguzi Mwandamizi kutoka Bodi ya Michedzo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Milao wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
unnamed2Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt.Kedmon Mapana (kushoto) akiwa katika banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akifafanua jambo wakati alipotembelea banda hilo wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Wa kwanza kulia ni Afisa Huduma wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA Njovu K. Njovu na anayefuatia ni Afisa Huduma wa Elimu kwa Mlipa Kodi TRA Serapio Luanda.
unnamed1Mwamuzi wa michezo ya sanaa za maonesho na Mhadhiri kutoka chuo Kikuu cha Dar es salaam Delphine Njewele (kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanasheria wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA) Hamisi Tika kwenye banda la PPAA wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe leo jijini Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
unnamedVijana wa Kikundi cha “Hisia Theatre Group” wakionesha ujuzi wao wa sarakasi wakati wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini leo Dar es salaam ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
================================================================

DICOTA WAMKABIDHI BALOZI LIBERATA MULAMULA RIPOTI YAO YA DICOTA CONVENTION 2014 ILIYOFANYIKA NORTH CAROLINA 

Viongozi wa DICOTA Lunda Asmani na Dr. Kurwa Nyigu walifika jioni ya Desemba 8, 2014 ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington DC kumkabidhi Mhe. Liberata Mulamula ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoka kati ya tarehe 2 mpaka 5.
Katika makabidhiano hayo yaliyo ambayo yalikua ni maelezo ya viongozi wa DICOTA na maoni ya wahudhuriaji wa mkutano huo wa kongamono wa ndani na nje ya Marekani ikiwemo DVD 2 ya mkutano huo.
Viongozi hao walimweleza Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwamba mkutano wa DICOTA COnvention 2014 ulikua wa mafanikio na kutokana na swala la uchaguzi mkuu mwaka 2015 mkutano wa kongamano wa DICOTA hautafanyika na matarajio yao ni kuufanya mwaka 2016 mji na jimbo bado haijajulikana. Pia bwn. Lunda Asmani alielezea DICOTA inavyojihusisha kwa karibu na viongozi wa Jumuiya za Watanzania wa majimbo nchini Marekani huku wakijaribu kuboresha mahusiano na baadhi ya viongozi wa Jumuiya ambao hapo nyuma ulilegalega.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula alianza kwa kuwashukuru viongozi hao kwa kupata wasaa wa kufika Ubalozini na kukabidhi ripoti na DVD na kusema alifurahi sana na mkutano wa DICOTA uliofanyika Durham, North Carolina kwani ulikua wa mafanikio  makubwa na ulitoa fulsa nyingi kwa wahudhuriaji wa mkutano huo mwaka huu. Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliwaasa viongozi wa DICOTA kuendelea kuwasiliana na wadhamini wa mkutano huo hasa walioweza kufika na kunadi bidhaa zao ili waweze kujua maendeleo ya bidhaa walizonadi kwenye mkutano huo akitolea mfano wa Azania Bank, NHC, PPF na wengine ambao wangependa kujua ni Watanzania wangapi nchini Marekani walionufaika na ujio wao kwenye mkutano huo. Kwa kufanya hivyo kunaleta mahusiano mazuri na wadhamini ili wasiishie hapo wazidi kuwatangza na wao kujitangaza kupitia mikutano ya DICOTA.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula aliendelea kwa kusisitizia viongozi hao kuendeleza mahusiano na Jumuiya za Watanzania nchini Marekani hususani viongozi wa Jumuiya hizo na kutafuta uwezekano wa kukutana nao mara kwa mara na akashauri Jumuiya zinapofanya mijumuiko yao na vyema na wao wakatuma mwakilishi kuhudhuria mijumuiko hiyo huku akitoa mfano wa sherehe za Uhuru zinafanyika kwenye majimbo toafauti ni vizuri DICOTA kutuma mwakilishi ili kuwa karibu na Jumuiya hizo pia kutajenga mshikamano wa karibu na Viongozi wa Jumuiya hizo.
Mwisho viongozi wa DICOTA waliuomba Ubalozi wasisite kuwaita mara wanapohitaji msaada wao kwani wanapotoa msaada kwa Ubalozi hujisikia kufarijika kwani ni furaha ni kutumia utaalamu na uzowefu wao katika kusaidia kusukuma kurudumu la maendeleo kwa kwa pamoja tunaweza.
 Viongozi wa DICOTA Lunda Asmani (kushoto)na Dr. Kurwa Nyigu wakitia saini kitabu cha wageni mara tu walipofika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC kuonana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamuala (hayupo pichani) na kumkabidhi ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA uliofanyika mapema mwezi wa Oktoba kwenye tarehe 2 mpaka 5 2014.
 Viongozi wa DICOTA Dr. Kurwa Nyigu (kushoto na Lunda Asmani(wapili toka kushoto) wakifanya mkutano wa makabidhiano ya ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 na Mhe. Liberata Mulamula akiwemo Afisa Ubalozi Switebert Mkama(kulia) jioni ya Jumatatu Desemba 8, 2014 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo barabara ya 22 NW, Washington, DC.
 Mkutano wa makabidhiano ukiendelea
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akimkabidhi Mhe. Balozi Liberata Mulamula Ripoti ya mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapama mwezi wa Oktoba Durham, North Carolina nchini Marekani.
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akitoa maelezo kwa Mhe. Balozi Liberata Mulamula kuhusiana na ripoti hiyo.
 Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiipitia kwa haraka haraka ripoti hiyo
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akimkbidhi Mhe. Balozi Liberata Mulamula DVD za mkutano wa kongamano wa DICOTA wa 2014 uliofanyika mapema mwezi Oktoba Durham North Carolina nchini Marekani.
 Kiongozi wa DICOTA Lunda Asmani akiemwelezea jambo mhe. Balozi Liberata Mulamula.
 Kiongozi Lunda Asmani akiendelea kuelezea jambo huku kiongozi mwenzake Dr. Kurwa Nyigu akimsikiliza.
Afisa Ubalozi Switebert Mkama akifuatilia mkutano wa makabidhiano wa ripoti ya DICOTA Convention 2014 uliofanyika Durham, North Carolina mapema mwezi wa Oktoba 2014.
=============================================================

FAINAL YA MASHINDANO YA WAZI YA TAIFA YA NGUMI YALIVYO MALIZIKA MWISHONI MWA WIKI UWANJA WA NDANI WA TAIFA

 Mabondia latifa Halidi  kushoto wa Kigoma na Vumilia Kalinga wa JKT wakioneshana umwanmba wa kutupiana makonde wakati wa mashindano ya taifa ya wazi yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita picha na SUPER D BOXING NEWS
Makamu wa Rais wa Shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini ‘BFT‘ Lukelo Willilo akimvisha medali ya dhaabu bondia Robert Kyaruzi baada ya kushinda katika fainal ya mashindano ya taifa ya wazi iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita
Mabondia Siwatu Elieta kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Zulfa Macho wakati wa fainali za mchezo wa masumbwi Macho alishinda kwa point mpambano huo
Mabondia latifa Halidi  kushoto wa Kigoma na Vumilia Kalinga wa JKT wakioneshana umwanmba wa kutupiana makonde wakati wa mashindano ya taifa ya wazi yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita picha na SUPER D BOXING NEWS
 
 Mfanya biashara na mdau na promota maarufu nchini Zahoro Maganga akisalimiana na bondia wakati wa fainaliya mashindano ya taifa

No comments:

Post a Comment