Idriss
Sultan Mtanzania aliyetikisa Bigbrother leo ameibuka mshindi wa
shindano hilo na kuwabwaga washiriki kutoka mataifa mbalimbali
yaliyoshiriki katika shindano hilo akiibuka na kitita cha shilingi
milioni 500 za Kitanzania katika shindano hilo lililokuwa likiendelea
kwa miezi mitatu nchini Afrika Kusini Idriss ni Mtanzania wa tatu
kushinda shindano hilo akitanguliwa na Mwisho Mwampamba na Richard wote
wakiwakilisha vizuri taifa la Tanzania katika shindano hilo,
===============================================================
WAZIRI CHIKAWE ACHANGISHA ZAIDI YA MILIONI 22 KKKT JIMBO LA KASKAZINI-MAGHARIBI NACHINGWEA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akifungua zoezi la uchangiaji wa harambee ya kupatikana
kwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi
linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi.
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo, anayefuata ni
Katibu Mkuu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini –Mashariki, Jane Mkimbo. Kulia
ni Mkuu wa Jimbo hilo, Mchungaji Charles Mtweve. Katika harambee hiyo
Shilingi Milioni 22.3 zilipatikana. Picha zote na Felix Mwagara
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akifungua zoezi la uchangiaji wa harambee ya kupatikana
kwa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi
linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi.
Katika harambee hiyo Shilingi Milioni 22.3 zilipatikana.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe akitoa mchango wake wa awali shilingi milioni moja kwa
ajili ya uchangiaji wa harambee ya kupatikana kwa shilingi milioni 100
kwa ajili ya ununuzi wa gari la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Jimbo la Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya
Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya
Nachingwea, Regina Chonjo, anayefuata ni Katibu Mkuu wa KKKT, Dayosisi
ya Kusini –Mashariki, Jane Mkimbo. Wapili kulia ni Mkuu wa Jimbo hilo,
Mchungaji Charles Mtweve. Katika harambee hiyo Shilingi Milioni 22.3
zilipatikana.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (watatu kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina
Chonjo (wanne kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la
Kaskazini-Magharibi, Nachingwea na KKKT Dayosisi ya Kusini-Mashariki,
Kanisa Katoliki na maofisa wa wilaya hiyo, mara baada ya kumaliza
harambee ya kuchangisha milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa gari la
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Jimbo la
Kaskazini-Magharibi linalojumlisha Wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na
Liwale mkoani Lindi. Picha zote na Felix Mwagara
===========================================================
DIAOMOND USIPIME ANOGESHA SHEREHE YA UHURU DMV
Prezida
wa Wasafi Diamond Platnumz akiwa pamoja na wacheza showa wake Roma
Tonsa na Moses Iyobo wakitoa burudani katika kunogesha sherehe ya miaka
53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika Sheraton Hotel ya Silver
Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na mashabiki wake kutoka
kila pembe ya Marekani huku mashabiki wengine wakitokea Tanzania, Picha
na Vijimabo Blog
Mzuka unazidi kupanda Diamond Platnumz asaula koti lake.
Balozi
akimshukuru Diamond kwa kuwezesha kunogesha usiku wa Uhuru wa Tanzania
na pia aliwashukuru wadhamini wa sherehe hiyo ya moaka 53 ya Uhuru wa
Tanzania Bara.
Diamond akizidi kuwapa burudani mashabiki wake
Shabiki akicheza wimbo wa mdogo mdogo
Shabiki akijumuika na Diamond kwenye jukwaa.
==========================================
WIMBO MPYA “ACHA MARINGO” wa KISS ft Rich Mavoko & Makomandoo
Msanii mpya kwenye gemu ya Bongo
Flava anayeitwa Abui Simon au la kimuziki ‘KISS’. Wimbo huo wewe ndio
utakuwa wa kwanza kuurusha hewani kwenye blogs kabla ya kuueleka kwenye
vituo vya redio siku ya Jumatatu.
Jina la wimbo ni ACHA MARINGO.
Ameutengeneza kwenye studio za SAY RECORDS, Kinondoni, Dar. Amewashirikisha Richie Mavoko na Makomando.
Natumai ushirikiano wako wa dhati, asante na Mungu akubariki.
Kaka Mwinyi – 0713 552211 au 0752 552211
================================================================
RAIS KIKWETE ATEUA MKUU MPYA MMOJA WA MKOA NA KUWAHAMISHA VITUO VYA KAZI WENGINE SITA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi wengine sita kuanzia jana, Jumamosi, Desemba 6, 2014.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Ndugu Ntibenda ataapishwa kesho, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.
Taarifa hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa Elaston Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa Simiyu ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine ni Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka Mkoa wa Arusha.
Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Desemba,2014
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
6 Desemba,2014
=================================================================
RAIS DR. SHEIN ASHIRIKI MAZIKO YA MUASISI WA CCM
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed
Shein (wa tatu kulia) akijumuika na waislamu na Viongozi kumuombea dua
Muasisi wa CCM Marehemu Mzee Juma Ameir Juma baada ya kumswalia katika
Msikiti wa Abdalla Rashid Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi na amezikwa
leo kijijini kwao Muungoni Wilaya ya Kusini Unguja.[Picha na Ikulu.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi AlhajDk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kulia) pamoja na Viongozi na Waislamu wakibeba Jeneza lenye mwili wa Muasisi wa CCM Marehemu Mzee Juma Ameir Juma baada
ya kumswalia katika Msikiti wa Abdalla Rashid Kiembesamaki Wilaya ya
Magharibi na kwenda kuzikwa leo kijiji kwao Muungoni Wilaya ya Kusini
Unguja,[Picha IKULU.] Wananchi
wakilibeba jeneza lenye mwili wa marehemu muasisi wa CCM marehemu Mzee
Juma Ameir Juma aliyefariki leo na kuzikwa kijijini kwao Muungoni Mkoa
wa Kusini Unguja,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein aliongoza maziko hayo,[Picha IKULU.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Balozi Seif Ali Iddi (katikati) pamoja na Waislamu na Wananchi mbali mbali wakishiriki katika Maziko ya muasisi
wa CCM Marehemu Mzee Juma Ameir Juma aliyefariki usiku wa kuamkia leo
na kuzikwa kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja.[Picha
IKULU.] Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitia udongo katika kaburi la muasisi
wa CCM Marehemu Mzee Juma Ameir Juma aliyefariki usiku wa kuamkia leo
na kuzikwa kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja.[Picha
IKULU.] Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitia udongo katika kaburi la muasisi
wa CCM Marehemu Mzee Juma Ameir Juma aliyefariki usiku wa kuamkia leo
na kuzikwa kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja.[Picha
IKULU.] Mjumbe wa Baraza la Wazee wa CCM Haji Machano akisoma wasifu wa muasisi wa CCM Marehemu Mzee Juma Ameir Juma baada ya mazishi yake yaliyofanyika leo kijijini kwao Muungoni wilaya ya Kusini Unguja mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.[Picha IKULU.]
======================================================
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA(TRA)WAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA NBAA
Naibu Waziri wa Fedha Adam
Malima akimkabidhi Tuzo kamishna mkuu wa TRA Rished Bade katika
kufunga mkutano wa mwaka wa wakaguzi na wahasibu (NBAA)
unaofanyika jijini Arusha ambapo TRA waliibuka kidedea katika tuzo za
bodi ya uhasibu na ukaguzi kwa kuongoza kundi la taasisi za serikali
kwa kutoa hesabu bora nchi nzima(Habari Picha na Pamela Mollel wa
Jamiiblog)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Clement Mshana akiwa anapokea tuzo kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha
Adam Malima baada ya kushinda katika uandaaji bora wa mahesabu
Naibu Waziri wa Fedha Adamu Malima akiwa anamkabidhi Mkurugenzi mkuu wa TANAPA Allan kijazi
tuzo kwa kushinda katika uandaaji wa mahesabu kiwango cha kimataifa
katika mfumo wa uandaaji wa viwango vinavyokubalika kimataifa
Mhasibu mkuu wa wizara ya
maliasili na utalii Layson Mwanjisi akipokea tuzo ya uandaaji bora wa
taarifa za mahesabu kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha Adamu
Malima
Mkurugenzi mkuu NBAA Pius Maneno akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima
Mwenyekiti wa bodi ya NBAA
Pro.Isaya Jairo akipokea zawadi kwa kufanikisha kuandaa mkutano mkubwa
wa mwaka wa wakaguzi na wahasibu (NBAA)
Naibu Waziri wa Fedha Adamu
Malima akimkabidhi Tuzo Mkaguzi mkuu wa ndani PPF Hosea Kashimba baada
ya kushinda kwa kuwa waandaaji bora wa taarifa za hesabu kwa mwaka 2013
Rais Kikwete afanya Kisomo Kumshukuru Mwenyezi Mungu Kwa Kupona
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mjukuu wake Ayman Ridhiwani
Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumalizika kisomo
cha shukran kwa Mwenyezi Mungu kiklichofanyika ikulu jijini Dar es
Salaam leo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya Mashekhe na wageni
waliohudhuria hafla ya kisomo maalum cha Kumshukuru Mwenyezi Mungu baada
ya kufanyiwa upasuaji na kurejea nyumbani salama kilichofanyika katika
viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam leo. Mjukuu
wa Rais, Ayman Ridhiwani Kikwete akicheza kwa furaha wakati Babu yake
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru wageni na Mashekhe
waliohudhuria hafla ya kisomo maalum kilichofanyika katika viwanja vya
ikulu jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro) Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mjukuu wake Ayman Ridhiwani
Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumalizika kisomo
cha shukran kwa Mwenyezi Mungu kiklichofanyika ikulu jijini Dar es
Salaam leo.
Tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne lafana TCC Chang’ombe
Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Dkt. Servacius Likwelile mara baada ya kuwasili viwanja
vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam ambapo linafanyika
tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne mwishoni mwa wiki
kuelekea maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Watumishi
wa wizara ya Fedha na taasisi zake wakiwa kwenye maandamano ya tamasha
la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne mwishoni mwa wiki kuelekea
maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Servacius Likwelile akimkaribisha Waziri wa
Fedha Saada Mkuya Salum kufungua tamasha siku nne (Disemba 6 hadi 7,
2014) la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne mwishoni mwa wiki
kuelekea maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akifungua tamasha la mafanikio ya Serikali
ya Awamu ya Nne mwishoni mwa wiki lililoandaliwa na Wizara ya Fedha kwa
kuandaa mashindano ya fani ya sanaa za maonesho yanayofanyika viwanja
vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Fedha Doroth Mwanyika wakati wa ufunguzi wa tamasha la mafanikio ya
Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC)
Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akimkabidhi cheti maalum cha ushiriki Mkuu
wa Kitengo cha mawasiliano Serikalini (GCU) Ingiahedi Mduma wakati wa
ufunguzi wa tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne
linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
Afisa
Uendeshaji PSPF Delphin Richard akikabidhiwa cheti maalum na Waziri wa
Fedha Saada Mkuya Salum cha ushiriki wa tamasha la mafanikio ya Serikali
ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe
jijini Dar es salaam. Wanakwaya
kutoka Wizara ya Fedha wakiimba wakati wa mashindano ya sanaa za
maonesho kwenye tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne
linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam
linaloshirikisha watumishi wa wizara hiyo na taasisi zake.
Kikundi
ncha ngoma kutoka Wizara ya Fedha wakicheza wakati wa mashindano ya
sanaa za maonesho kwenye tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya
Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es
salaam.
Kikundi
cha shairi kutoka Wakala ya Huduma ya Manunuzi Serikalini (GPSA)
wakiimba shairi wakati wa mashindano ya tamasha la mafanikio ya Serikali
ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja vya Sigara (TCC) Chang’ombe
jijini Dar es salaam.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwaaga watumishi mara baada ya kufungua
tamasha la mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Nne linalofanyika viwanja
vya Sigara (TCC) Chang’ombe jijini Dar es salaam.
==================================================================
Timu ya Kriket ya Uganda yatua nchini kwa udhamini wa Fast Jet
Wachezaji
wa timu ya Kriket ya Uganda wenye umri wa chini ya miaka 19 wakiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (juzi)kutokea
Kampala, Uganda kwa ziara ya siku tano ya mchezo huo hapa nchini chini
ya udhamini wa Kampuni ya ndege ya Fast Jet
Wachezaji
wa timu ya Kriket ya Uganda wenye umri wa chini ya miaka 19 wakiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (juzi)kutokea
Kampala, Uganda kwa ziara ya siku tano ya mchezo huo hapa nchini chini
ya udhamini wa Kampuni ya ndege ya Fast Jet
Baadhi
ya wachezaji wa timu ya Kriket ya Uganda wenye umri wa chini ya miaka
19 wakihokiwa na waandishi wa habari baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Wachezaji
wa timu ya Kriket ya Uganda wenye umri wa chini ya miaka 19
wakijadiliana jambo muda mfupi baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kutokea Kampala, Uganda kwa ziara ya
siku tano ya mchezo huo hapa nchini chini ya udhamini wa Kampuni ya
ndege ya Fast Jet
=================================================================
Tigo ilivyowafikia wateja wake katika tamasha la Nyama Choma Festival
Mfanyakazi
wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Rayu Othman (kushoto)
akimhudumia mteja aliejitokeza kwenye banda lao kujipatia huduma za
kampuni hiyo wakati wa Tamasha la Nyama Choma lililofanyika jana katika
viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mfanyakazi
wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Prisila Elifas (kushoto)
akiwahudumia wateja waliojitokeza kwenye banda lao kujipatia huduma za
kampuni hiyo wakati wa Tamasha la Nyama Choma lililofanyika jana katika
viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Sehemu
ya banda la Tigo kama linavyoonekana kwa mbele katika Tamashala la
Nyama Choma lililofanyika jana katika viwanja vya Chuo Kikuu Dar es
salaam.
Wafanyakazi
wa kampuni ya simu ya Tigo wakiwa na wateja katika banda lao wakati wa
Tamasha la Nyama Choma lililofanyika jana katika viwanja vya Chuo Kikuu
Dar es Salaam.
Wafanyakazi
wa kampuni ya simu ya Tigo wakiwa na wateja katika banda lao wakati wa
Tamasha la Nyama Choma lililofanyika jana katika viwanja vya Chuo Kikuu
Dar es Salaam.
=====================================================================
MKUTANO WA KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA (NEC)
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu
wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu
ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja katika Mkutano wa Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) leo,[Picha na Ikulu.] Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Chama
cha Mapinduzi CCM alipowasili katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM
Kisiwandui Mjini Unguja katika Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri
Kuu ya CCM Taifa (NEC) [Picha na Ikulu.]
/Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais
wa Zanzibar pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi
(kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai (kulia)
wakiwa katika kikao cha siku moja cha Mkutano wa Kamati Maalum ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kilichofanyika leo katika ukumbi wa
Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] Wajumbe
wa Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)
wakiwa katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja
ulipofanyika mkutano huo leo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.]
Wajumbe
wa Sekretarieti wa Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM
Taifa (NEC) Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM
Kisiwandui Mjini Unguja wakiwa tayari kuweka kumbu kumbu kwa mabo yote
yatakayozungumzwa katika Mkutano huo uliofanyika leo chini ya Mwenyekiti
wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, [Picha na Ikulu.] Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa taarifa kwa Wajumbe wa
Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya (NEC)
katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja kiako hicho
kilifanyika leo chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali
Mohamed Shein(katikati) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar pia Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi (kushoto), [Picha na
Ikulu.] Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiendesha Kikao cha siku moja cha
Mkutano wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)
kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini
Unguja (kushoto) Makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar pia Mjumbe wa kamati
Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi na (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,[Picha na Ikulu.]
===============================================================
MAMA SALMA KIKWETE AFANYA MIKUTANO YA KAMPENI KATA ZA NACHINGWEA NA MINGOYO HUKO LINDI
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
anayewakilisha Wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akisalimiana na
viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea iliyoko mjini Lindi wakati
alipotembelea tawini hapo kwa ajili ya kikao na viongozi wa kata hiyo
juu ya ushiriki wa Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi wa serikali za
mitaa, vjiji na vitongoji unaotarajiwa kufanyika tarehe 14.12.2014. Viongozi
wa CCM Kata ya Nachingwea pamoja na wagombea uongozi kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa wakiwa katika kikao na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa Mama Salma Kikwete (hayupo pichani).
Mjumbe
wa NEC Taifa wa CCM na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki katika
shamrashamra na viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea muda mfupi kabla ya
kuzungumza na viongozi hao tarehe 6.12.2014.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa Chama Cha Mapinduzi, Mama Salma
Kikwete akiwahutubia viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea na wagombea wa
chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika
tarehe 14.12.2014.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa Chama Cha Mapinduzi, Mama Salma
Kikwete akiwahutubia viongozi wa CCM Kata ya Nachingwea na wagombea wa
chama hicho kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika
tarehe 14.12.2014. Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya CCM, Mama Salma Kikwete akimjulia
hali mtoto mdogo aliyebebwa na mama yake wakati Mama Salma akiingia
kwenye sehemu ya mkutano wa kampeni katika Kata ya Mingoyo huko Lindi
tarehe 6.12.2014. Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma
Kikwete akijumuika na viongozi mbalimbali wa Mkoa na wilaya ya Lindi
mjini pamoja na wananchi wa Kata ya Mingoyo kucheza wakati wa mkutano wa
kampeni uliofanyika Mnazi Mmoja tarehe 6.12.2014.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma
Kikwete akijumuika na viongozi mbalimbali wa Mkoa na wilaya ya Lindi
mjini pamoja na wananchi wa Kata ya Mingoyo kucheza wakati wa mkutano wa
kampeni uliofanyika Mnazi Mmoja tarehe 6.12.2014.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Kata ya Mingoyo pamoja na
wananchi wa Mnazi Mmoja wakati wa mkutano wa kampeni ya uchaguzi wa
serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 14,12.2014
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi wa Kata ya Mingoyo pamoja na
wananchi wa Mnazi Mmoja wakati wa mkutano wa kampeni ya uchaguzi wa
serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 14,12.2014
PICHA NA JOHN LUKUWI.
===============================================================
BELLA AITIKISA DAR LIVE USIKU WA NANI KAMA MAMA
Mfalme
wa masauti, Christian Bella ‘Obama’ akifanya yake usiku wa kuamkia leo
Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.
Nyomi
ya mashabiki walijitokeza katika uzinduzi wa albamu yake mpya ya Nani
Kama Mama ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Madansa wa Malaika Music bendi wakifanya yao.
Mashabiki wakicheza na Christian Bella ‘Obama’.
Mashabiki wakiwa wamepagawa na shoo ya mfalme wa masauti, Christian Bella ‘Obama’ (hayupo pichani).
Christian Bella ‘Obama’ akizidi kuwapagawaisha mashabiki wake.
Madansa wa Christian Bella wakifanya yao.
Mashabiki wakicheza na kuimba wimbo wa Nakuhitaji wa Bella.
Bella na wacheza shoo wake wakifanya yao.
Christian Bella akiimba wimbo wa Nani Kama Mama akiwa na shabiki wake.
BENDI ya muziki wa Dansi ya
Malaika chini ya Christian Bella ‘Obama’ usiku wa kuamkia leo iliutikisa
Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar
baada ya kuwapagawisha mashabiki kwa shoo ya nguvu.
Onyesho hilo lililoanza saa
tatu usiku ambapo Malaika bendi walikuwa wakiwapa ladha mashabiki kwa
kupiga kopi mbalimbali ya nyimbo za Kikongo zinazobamba.
Ilipofika saa nne na nusu
ukumbi ulilipuka kwa shangwe baada ya kiongozi wa bendi hiyo Christian
Bella kupanda jukwaani kwa wimbo wake wa Yako Wapi Mapenzi ambao
ulisababisha mashabiki kuinuka katika viti vyao na wale ambao walikuwa
wakinyemelewa na usingizi kuamka.
Bella alizidi kuwapagawisha
mashabiki kwa kupiga nyimbo kali mfululizo ambazo zinatamba katika redio
na vyombo mbalimbali vya habari ukiwemo Nani Kama Mama, Yako wapi
Mapenzi, Msaliti, Usilie na nyingine kibao.
(PICHA/HABARI: ISSA MNALLY/ GPL)
==========================================================
Washindi wa Maonesho ya Keki Wapatikana Dar
JOPO la Majaji watatu na mabingwa
wa fani za mapishi leo wamewatangaza mabingwa wa utengenezaji keki
waliojitokeza katika Maonesho ya bidhaa za keki ‘Azam World of Cakes
Exhibition’ yaliofanyika katika Hoteli ya Serena ya jijini Dar es
Salaam.
Jumla ya makampuni na watengenezaji keki wapatao 39 wameshiriki katika maonesho hayo ya keki yalioandaliwa na kampuni ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania.
Jumla ya makampuni na watengenezaji keki wapatao 39 wameshiriki katika maonesho hayo ya keki yalioandaliwa na kampuni ya Insights Productions Limited kwa udhamini wa Kampuni ya Azam Tanzania.
Akitangaza washindi katika
maonesho hayo ya keki, mmoja wa majaji ambaye pia ni Mpishi Mkuu, toka
Ramada Encore ya jijini Dar es Salaam, Edward Mukabana alisema timu ya
majaji hao imewapata washindi wa kwanza watatu katika makundi matatu;
yaani mshindi wa Keki yenye Radha Bora, Mbunifu Bora wa Keki na Mshindi
wa Keki yenye Mvuto Kimuonekano.
Jaji huyo wa ‘Azam World of Cakes
Exhibition’ aliwataja Amina Salim kuwa ndiye aliyeibuka mshindi wa keki
yenye radha bora zaidi, huku kampuni ya Beta Bakery ikitwaa taji la
mbunifu Bora wa Maonesho hayo ya keki. Pia alimtangaza Janeth Muawiriro
kuwa ndiye mshindi wa keki yenye Mvuto kimuonekano katika washiriki
wote.
Jopo hilo la majaji wa ‘Azam World
of Cakes Exhibition’ pia lilimtangaza Leila Dhiyebi kuwa ni mshindi wa
kwanza aliyepigiwa kura na wananchi waliotembelea maonesho hayo makubwa
ya keki Tanzania. Kundi lingine la washindi ambao keki zao ziliwavutia
majaji ni pamoja na Haika Shao na Caroline Gul pamoja na wanae wawili
ambao walishiriki kubuni umbo la keki kwa mchoro iliyotengenezwa na
mamayao.
Akizungumza awali kabla ya
kuwatangaza washindi, Jaji Mkuu wa Mashindano hayo ya ‘Azam World of
Cakes Exhibition’, Tom Owino (Excetive Chef) alisema walisema
wamezipitia keki zote za washiriki kuangalia vigezo mbalimbali vya
upishi, muonekano na kuonja radha ya kila keki kabla ya kukaa chini na
kuanza kufanya maamuzi ya pamoja ya majaji kwa kuzingatia vigenzo vya
msingi katika utengenezaji keki.
Aidha kwa upande wake, Marion
Elias Mkurugenzi wa Kampuni ya Insights Productions Limited, ambaye pia
ni Mratibu wa maonesho hayo alisema maonesho hayo yamekuwa na mvuto
baada ya kushirikisha makampuni na watu binafsi huku yakilenga kutangaza
bidhaa nzima ya keki na ubunifu katika utengenezaji.
Alisema washiriki wote wamepata
fursa ya kubadilishana uzoefu na kujifunza ubunifu zaidi wa shughuli
hizo toka kwa wataalam wengine jambo ambalo litawabadili kwa namna
fulani, ikiwa ni pamoja na kupata zawadi toka kampuni ya Azam na vyeti
maalum vya kutambua mchango wao kiushiriki.
Kwa upande wake Mratibu wa
Matangazo na Uhusiano wa Umma toka Kampuni ya SSB, Mohammed Ramadhan
alisema Azam ikiwa ni kampuni inayotengeneza unga bora wa kutengenezea
keki imeamua kudhamini ikiwa ni ishara ya kutambua taaluma hiyo ya
utengenezaji wa keki nje na ndani ya Tanzania. Wananchi walipata fursa
ya kuangalia keki mbalimbali pamoja na kuonja radha zake jambo ambalo
lilileta mvuto zaidi kwa washiriki.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
=======================================================================
WANAFUNZI 1,044 WAHITIMU CHUO KIKUU ARDHI
Wahitimu wa digrii ya elimu jamii
katika taaluma za maendeleo jamii wakishangilia baada ya Mkuu wa Chuo
Kikuu Ardhi (ARU), Cleopa Msuya kuwatunuku katika mahafali ya 8 ya chuo
hicho, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam jana.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU),
Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Rigobert Buberwa, wakati wa
mahafali ya 8 ya Chuo hicho, Dar es Salaam. Buberwa ametunukiwa digrii
hiyo baada ya kufanikiwa kufanya utafiti unaohusu “Kuelekea modeli ya
mfumo wa kompyuta wa kutunza taarifa za ardhi na mabadiliko ya umiliki
wake: Nyenzo mpya ya Usimamizi wa Ardhi nchini Tanzania.
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU),
Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu (Doctor of Phylosophy Degree),
Deusdedit Kibassa, wakati wa mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika
kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo.Mada ya utafiti
aliyoifanya inahusu: “Umuhimu wa kutumia maeneo ya kijani kupunguza
athari zitokanazo na kuongezeka kwa hali ya joto katika maeneo ya
katikati ya Jiji la Dar es Salaam.”
Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi (ARU),
Cleopa Msuya akimtunuku Digrii ya Uzamifu, Dawah Mushi, wakati wa
mahafali ya 8 ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee, Dar es Salaam. Mada ya utafiti aliyoifanya Mushi inahusu:
“Uhamishwaji wa makazi ya watu wengi waliobomolewa makazi yao katika
mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam.”
Daniel Mbisso akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Joel Msami akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Eliwaha Msangi akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Margareth Ntiyakunze akitunukiwa Digrii ya Uzamifu
Sara Phoya akitunukiwa digriii ya uzamifu
Baadhi ya wahitimu wakipiga picha wakati wa mahafali hayo
Bendi ya JKT ikiongoza maandamano ya viongozi na wahadhili wa chuo hicho kuingia ukumbini
Wahadhiri na viongozi wakiingia kwa maandamano kwenye ukumbi
baadhi ya wahitimu wakisubiri kutunukiwa digrii
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Ardhi, Tabitha Siwale akihutubia katika mahafali hayo
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrissa Mshoro akihutubia wakati wa mahafali hayo
Wahitimu wa Chuo Kikuu Ardhi
(ARU), wakiweka kofia kichwani ikiwa ni ishara ya kutunukiwa digrii ya
uzamili ya sayansi ya usimamizi na uchumi ujenzi, wakati wa mahafali ya 8
ya Chuo hicho, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es
Salaam
Ni furaha iliyoje baada ya kutunukiwa
Baadhi ya ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu wakiwa katika mahafali hayo
Waziri Mkuu wa zamani, ambaye ni Mkuu wa Chuo cha ARU, Cleopa Msuya akitoka baada ya mahafali hayo kumalizika leo
Msuya akiongoza maandamano kutoka nje baada ya mahafali hayo kumalizika
Hali ilivyokuwa nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya mahafali kumalizika
===========================================================
MASHINDANO YA MICHEZO YA WABUNGE WA AFRIKA MASHARIKI YAANZA JIJINI ARUSHA
Maandamano ya mashindano ya michezo ya wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),jijini Arusha ambayo yanatimua vumbi Uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwanzia tarehe 6 hadi 12 mwezi huu
Wabunge wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania wakifwatilia ufunguzi rasmi wa bonanza la mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kulia ni kiongozi wa timu ya bunge la Tanzania Idd Azan katikati ni Mh.mbunge Stevin Ngonyani a.k.a Maji marefu
Mbunge wa Arumeru Mashariki,
Joshua Nassari akifurahia ushindi baada ya kushinda nafasi ya kwanza
kupeperusha vema bendera ya Tanzania baada ya kuibuka mshindi mbio za
mita 100 akifuatiwa na Isaac Melley wa Kenya na Tom Aza wa Uganda
aliyeshika nafasi ya tatu.
Wabunge wa Tanzania Halima Mdee
na Ester Matiko waliendeleza ubabe wa bunge la Tanzania dhidi ya wenzao
baada ya kushika nafasi ya kwanza na pili katika mbio za mita 1,500 na
kuwaacha wenzao kutoka Uganda, Kiiza Winfred na Kangi Elizabeth
wakishikilia nafasi za tatu na nne.
Mbunge Ester Matiko wa Tanzania
akijiandaa kukimbia mbio za mita 400,ambapo aliwatimulia vumbi wabunge
wenzake kutoka Kenya, Uganda na bunge la Afrika Mashariki (Eala).
Kaimu Spika wa bunge la EALA Chris Opoka akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo
Mkuu wa wilaya Arumeru Mhe Nyirembe Munasa
afungua mashindano ya michezo kwa wabunge ambapo aliwataka wachezaji
kuacha kuamini imani za kishirikina na badala yake wamtegemee Mungu
kwani michezo ni kazi kama ajira nyingine
Mkurugenzi wa KeyMedia Agency
Limited Bi Anna Lazaro akiwa na wabunge wa Tanzania leo jijini Arusha
katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoandaliwa na EALA(East
African Legislative Assembly)
Katikati Mkurugenzi wa KeyMedia
Agency Limited Bi Barbra Lazaro akiwa na wabunge wa Tanzania leo jijini
Arusha katika mashindano ya michezo mbalimbali yaliyoandaliwa na
EALA(East African Legislative Assembly)
Aliyevalia t-shart ya njano ni designer mkuu wa kampuni ya KeyMedia Agency Limited Bahati Masawe akiwa na waheshimiwa Wabunge
Mbunge wa EALA kutoka nchini Tanzania Mh.Twaha Taslama akiwa anavuta kamba wakati wa mashindano ya hayo
Mbunge wa Kenya akiwa amebebwa juju baada ya kushinda katika mbio za mita 100
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, Ester Bulaya akiwa anashangilia kwa furaha katika mashindano hayo
No comments:
Post a Comment