Wagonjwa wadaiwa kunyanyaswa kingono katika hospitali za Uingereza.
Mlipuko wa kisiri wa unyanyasaji wa
kingono katika hospitali za Uingereza umegunduliwa huku takwimu mpya
zikionyesha zaidi ya mashambulizi 1600 yaliripotiwa kwa polisi katika
kipindi cha miaka mitatu iliopita.
Kumbukumbu zilizopatikana na gazeti la
The Guardian chini ya sheria ya uhuru wa habari zinaonyesha ongezeko la
asilimia 50 ya ripoti za unyanyasaji wa kingono kwa kutumia nguvu katika
hospitali tangu mwaka 2011.
Unyanyasaji huo unashirikisha visa 157
vya ubakaji.Takwimu za unyanyasaji huo katika hospitali zilitolewa na
vituo 38 vya polisi kati ya vituo 45 nchini Uingereza.Wagonjwa hospitaliniRipoti hiyo inadai kuwa mashambulizi 1,615 yanayojulikana yanafanyika katika kliniki za kibinafsi,na vituo vyengine vya afya.
Lakini viongozi wa mashtaka wanasema
kuwa hadi asilimia 90 ya visa vya unyanyasaji haviripotiwi swala
linaloonyesha kwamba takwimu za ukweli huenda ziko juu zaidi.
No comments:
Post a Comment