MWENYEKITI wa klabu wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji, ameagiza Polisi ‘Marafiki’ kuwakomesha Baada ya
kumtimua kocha Mkuu wa timu yake
na baada ya kubwaga chini sekretariati ya klabu hiyo, Mwenyekiti wa
Klabu ya Young Africans Sports Club (Yanga)
Bw, Yusuf manji, ameamua
kuwafanyizia baadhi ya waliokuwa watumishi wa Klabu hiyo akiwemo Beno
Njovu, Katibu Mkuu aliyepita.
Wakandamizwe haswa kulingana na
mawasiliano yaliyonaswa na makachero wetu kati ya Mwenyekiti huyo na
viongozi wa juu wa Klabu hiyo, Manji amewapa maelekezo wanasheria wake
na Sekretariati ya sasa kuwafungulia mashtaka Sekretariati iliyopita
kwa madai ya ufujaji pesa, huku akiwataka viongozi hao kutumia
‘marafiki’ zao waliooko katika jeshi la polisi ‘kuhakikisha
wanashugulikiwa.
Katika mawasiliano hayo kupitia email ya tarehe 22 Desemba ,
Manji pia anamwagiza mtu
aliyetambulika kuwa mhasibu anayaenda kwa jina la Amit kugharamia
‘maagizo hayo yote’, na kumpa taarifa kila siku. Vyombo vya habari
kutumika Manji pia ameagiza wafanyakazi hao wazamani ‘wachafuliwe’
kupitia kampeni kali magazetini, huku akielekeza ‘Press Release’ yenye
saini yake itolewe ikionesha ‘masikitiko
yake’.
Adhabu mbele, hukumu nyuma Huku
akitoa maagizo wafanyakazi hao washugulikiwe ipasavyo na polisi
‘marafiki’ zake, Bwana Manji ametupilia mbali haki za wafanyakazi hao
kusikilizwa kukiwa hakuna uchunguzi wowote uliokwishafanyika kuhusu
madai yake dhidi ya watumishi hao zaidi ya hisia zake mwenyewe na
Sekretariati mpya inayotekeleza kila alitakalo bila kuhoji.
Maagizo yazua mpasuko ndani ya kamati tendaji
Kufuatia maagizo ya Manji, mmoja wa watumishi wapya
aliyetambulika kama Frank Chacha alitekeleza maamuzi hayo ambayo
mwenyekiti huyo alikuwa amesema hayapingiki wala hayahojiki kwa email
yake, huku wakifungua kesi katika kituo cha Polisi kati Dar es salaam na
kufanikiwa kuweka wafanyakazi wawili ndani huku wakiendelea kumuwinda
Beno Njovu Lakini masaa machache baada ya hatua hizo, kuna dalili kuwa
baadhi ya viongozi ndani ya klabu hiyo wanapinga vikali hatua hizo za
Manji na wametishia ‘kuaachia’ ngazi.
Mpasuko huo ndani ya Yanga umedhihirishwa na email kutoka kwa
Bwana Omar, Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala akimjulisha Manji kuwa
jana Jumanne, baada ya kutekeleza maagizo ya Mwenyekiti huyo alipokea
simu kutoka kwa Isaac Chanji, mjumbe wa
Kamati Tendaji akitishia kuwa
hatua ambazo zilikuwa zimeshachukuliwa zilikuwa za hatari kwa Klabu hiyo
na kuwa yeye Chanji na wajumbe wengine wengelazimika kuwaachia akina
Omari na Chacha timu hiyo.
Kikosi kazi cha Fullshangwe
kilipomtafuta Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji Simu yake ilikuwa
ikiita bila majibu lakini hakikuishia hapo kilitafuta msemaji wa Klabu
hiyo Bw. Jerry Muro ambaye alijibu kwamba kesi hiyo inawahusu
wafanyakazi wa zamani wa Yanga hivyo yeye hawezi kuzungumzia zaidi
lakini shauri hilo lileripotiwa polisi na baada ya uchunguzi wa poilisi
taarifa rasmi kuhusu tuhuma zinazowakabili wafanyakaizi hao wa klabu ya
Yangza wa zamani itatolewa na jeshi hilo.
……………………………………………………………………….
Maswali Tata
Kufuatia hatua hii ya Manji mtu
unaweza kujiuliza maswali kadhaa: Je kwa nini Yanga inakuwa na kesi kila
wakati? Gharama za kesi hizi, ambazo nyingine siyo za lazima, si mzigo
usiokuwa na faida kwa Yanga? Mara
wachezaji, makocha, na Sekretariati za nyuma.
Ni dhahiri kuwa hata kama kesi
hii ya sasa ina msingi wowote, basi uchunguzi ungetangulia. Lakini,
labda kwa jeuri ya hela, Manji ameshawahukumu watumishi wale na ni wazi
kuwa yuko tayari hata kupindisha sheria ili afikie lengo lake. Lengo la
Manji hasa ni nini? Anajaribu kuwaadhibisha hawa watumishi kweli au ni
kujenga hoja za Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo unaotegemewa kufanyika
Januari 2015 kwa
kujenga mazingira ya kuwasahaulisha wanachama wa Yanga baadhi ya ahadi alizotoa na ambazo hadi sasa
bado ni ahadi hewa tu?
No comments:
Post a Comment