Baraza
la Usalama la Umoja wa mataifa limekataa azimio lililoandaliwa na
Palestina ambalo limewasilishwa na Jordan linalopendekeza kusitishwa kwa
mpango wa Israel wa kuyakalia maeneo ya Palestina kwa miaka miaka
mitatu.
Jordan iliwasilisha azimio hilo baada ya kukubaliwa na nchi 22 za kiarabu ikiwemo mamlaka ya Palestina.Kura tisa zilihitajika ili kupitisha azimio hilo lakini azimio hilo lilipigiwa kura nane pekee.
Nchi mbili zilipiga kura ya hapana kupinga azimio hilo ambazo ni Australia na Marekani zilizokataa mpango huo wa mwisho na kusema hautasaidia katika masuala ya usalama wa Israel.
Nchi tano hazikupiga kura ambazo ni Uingereza, Lithuania, Nigeria, Jamuhuri ya Korea na Rwanda, huku Urusi, China, Ufaransa, Argentina, Chad, Chile, Jordan na Luxembourg zikilipigia kura ya ndio azimio hilo.
No comments:
Post a Comment