Mwanamme
mmoja raia wa Uturuki aliyempiga risasi na nusura amuue aliyekuwa
kiongozi wa kanisa katoliki papa John Paul wa pili mwaka 1981 ameweka
maua kwenye kaburi lake katika makao makuu ya kanisa katoliki ya
Vatican.
Ziara ya Mehmet Ali Agca kwenye makao ya Vatican
inafanyika miaka 30 tangu John Paul amtembelee gerezani na kumsamehe kwa
kujaribu kumuua.
Bwana Agca aliomba kukutana na kiongozi wa sasa wa kanisa katoliki papa Francis lakini hata hivyo ombi lake lilikataliwa
Aliachiliwa
kutoka gerezani nchini Italia mwaka 2000 na kisha baadaye akatumikia
kifungo chengine cha miaka 10 nchini Uturuki kwa makosa tofauti.
Hadi sasa sababu zake za kutaka kumuua papa John Paul hazijulikani.
No comments:
Post a Comment