Na:Mwandishi wetu
Kampuni ya Inter
Quality Traders ya jijini Dar es Salaam,na ambayo inamilikiwa na Mzalendo wa
Kitanzania, Emmanuel Elisante, imetoa OFA YA PUNGUZO LA BEI ZA HOSTELI ZILIZOPO KIJITONYAMA DAR ES
SALAAM, kwa wanafunzi wanaoingia kwa mara ya kwanza kulipia kuanzia miezi 4 na
kuendelea tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni kuanzia miezi 8.
MKURUGENZI MKUU wa Inter Quality Traders, Bwana Emmanuel
Elisante, amesema kuwa ofa hizo ni kwa
Wanafunzi wanaoingia kwa mara ya kwanza, kwa lengo la kuwapa unafuu wa maisha
wakati wakiendelea kujipanga, “Hostel ni za kisasa na kwa Bei Nafuu kabisa,
kama zilivyo ni tofauti na Huduma za Hosteli zingine, maeneo ni mazuri Sinza
Mori, Nyuma ya Jengo la Sayansi na Teknolojia na pia Barabara ya Mapambano Kijitonyama, kwa mwaka huu kutokana na
changamoto zinazotukabili na kulikabili Taifa, nimeamua kuchukua uzalendo
kwanza wa kuwajali wanafunzi,natoa ofa kwa wale wote wanaoingia kwa mara ya
kwanza kulipia ada ya miezi 4 badala ya miezi 8, lakini pia baada ya kukaa na
kuzungumza na wanafunzi waliopo, pamoja na mambo mengine ya huduma za hostel
walihitaji pia kuweza kuunda timu zao na kuwa na Jezi ili wawe na timu
itakayokuwa ikicheza na timu mbali mbali.
Hosteli hizo zinakidhi
Mahitaji ya Wasomi hususani wa Vyuo mbali mbali kwa kuwa HOSTELI hizo
zinapatikana Maeneo ya Karibu na Barabara kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi
kupata Usafiri kwa Urahisi na kuongeza kuwa Tatizo la Usafiri kwenye Hosteli
hizo hakuna.
Lakini katika Hizo
HOSTELI hakuna tatizo la Maji, Hakuna tatizo la Umeme kutokana na kuwepo kwa
mitambo ya Maji pia Generator kubwa kwa ajili ya kusaidia pale Umeme unapokuwa na
tatizo.
Akizungumza na
waandishi waliofika kukagua Hosteli hizo Elisante, alisema kuwa dhumuni la
kuanzisha hizo HOSTELI inatokana na changamoto zilizokuwa zinawakabili
wanafunzi wa USTAWI wa Jamii, Chuo cha Ardhi, Royal College, Kilimanjaro
College Kwa Mama Ngoma, Chuo cha Kodi (ITA), CBE, na wengine wengi wanaosoma kwenye maeneo ya
JIJI la Dar es Salaam kuwa na hitaji hilo.
“Hizi Hosteli kama
mnavyoona wenyewe ni salama kwa Usalama wa Wanafunzi wanaoishi hapa, Ulinzi ni
wa Uhakika kama mnavyoona, na pamoja na yote tunatambua Umuhimu wa Umeme na
Maji kwa hawa wasomi, kwa hiyo masuala hayo tumeyajengea Misingi Imara ya
kuhakikisha kwa miaka 8 iliyopita na kwamba wakati wote mahitaji hayo
yanakuwapo, lakini pia nimetoa Punguzo la Bei kwa Mwaka huu 2015 kwa kuwa ni
mwaka wa upanuzi mkubwa wa hosteli zetu, kwa hiyo nimeamua wateja wetu
washiriki baraka hii kwa kuwapa Punguzo Vijana wetu ili waweze kutumia mwanya
huo kujipanga vizuri kwa lengo la kukabiliana na Elimu na mafanikio kimaisha
kwa ujumla.
Hosteli hizo ambazo ni
za kwanza kuwa na Mfumo wa ushirikishwaji wa pamoja katika Michezo, wanafunzi
kwa jinsia zao wameunda timu za michezo kwa lengo la kuwa na timu zao
zitakazokuwa zinashiriki michezo mbali mbali kwa lengo la kuwafanya wanafunzi
kukutana kati yao na wadau mbali mbali.
Pia tumeamua kuwa na
timu zetu za michezo kwa wanafunzi wanaoishi hapa, kwa kuwa ni wengi itakuwa ni
jambo zuri maana lengo ni wao waishi kama wanafunzi wa chuo kimoja ama watoto
wa baba mmoja, na hii itawaunganisha vizuri na kuwapa nguvu na akili zaidi.
Kuhusu vyumba kwenye Hosteli
hizo zimegawanywa kutokana na wahitaji wenyewe, kuna vyumba vya watu wane yaani
vitanda double 2 na watu 6, vitanda
double 3, vyenye nafasi kubwa kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kujisomea.
Jambo lingine ni uwepo
wa Mazingira ya kujisomea yaliyotengenezwa mahususi kukidhi haja za wasomi hao,
ambapo kuna Jukwaa kwa ajili ya kusomea usiku na wakati wote bila bughuza
yoyote.
Chakula pia
kinapatikana kwa bei nafuuu maeneo yote ya hizo hosteli kutegemeana na hitaji
la mwanafunzi na chakula anachopenda kutumia kwa wakati huo.
Hosteli hizo zinakidhi
mahitaji ya wanafunzi mbali mbali wa jiji la Dar es Salaam, kwa Maana Usafiri
wa kutoka maeneo hayo ni mwingi na wa haraka kumwezesha mwanafunzi kuwahi
Masomo popote Pale.
Kwa Mawasiliano kuhusu
hizo Hosteli tupigie namba hizi hapa.
+255-713-276982/+255784125433/+255715301794/+255-767-869133. WOTE
MNAKARIBISHWA.
No comments:
Post a Comment