Shirika
la ndege la AirAsia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta
ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za
ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini
Indonesia.
Zadi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.
Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta
No comments:
Post a Comment