Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix
Ntibenda wa pili kulia akikabidhi hundi ya shilingi milioni 17na laki
tano kwa wajasiliamali wa MT meru curios &crafts market
wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vijago jijini walizo kopa kwa
ajili ya kufanya biashara kabla wa soko lya kunguliwa na soko hilo
mapema mwezi uliopita
Meneja wa taasisi hiyo Baraka Jekonea akiongea na vyombo vya habari
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda akiongea katika halfa hiyo
=======================================================
Na:Pamela Mollel
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda ameipongeza taasisi
inayotoa huduma za kifedha (FINCA)kwa kuwafutia zaidi ya milioni 30
wanachama 35 wajasiliamali wa MT meru curios &crafts market
wanaojishughulisha na uzaji wa bidhaa za vinyago hela walizo kopa kwa
ajili ya kufanya biashara kabla ya soko loa kunguliwa mapema mwezi
uliopita.
Ntibenda alisema hayo jana wakati akikabidhi hundi ya
shilingi milioni 17na laki tano kwa wajasiliamali hao mbele ya
waandishi wa habari iliyofanyika eneeo la soko hilo lililoko wilaya ya
arusha mkoa wa arusha.
Kwa upande wa meneja taasisi hiyo Baraka Jekonea alisema
kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kuendeleza ujenzi wa soko hilo I
benki hiyo in warudi katika hali yao ya zamahi ya biashara .
“Sisikama Taasisi ya Kifedha Finca tumeamua kuwasaidia ili
tuweze kuwanusuru wahanga hawa kwa janga walilolipata tunaimani kwamba
watarejea katika hali yao ya zamani kwani tangu wakumbane na changamoto
hiyo maisha yao yamekuwa magumu sana”alisema Jekonea
Pia alitoa wito kwa
wafanyabiashara ambao hawajajiunga na taasisi hiyo kufanya hivyo kwa
kuwa benki hiyo inajali wajasiriamali na kuwataka kujiunga na taasisi ya
mikopo ili kuweza kupata mikopo ya nafuu.
Kwa upande wake Kaimu
Mwenyekiti wa soko hilo Hamis Juma alishukuru taasisi kwani pesa hiyo
itawasaidia sana sana katika kujikwamua na kurejesha hali yao ya awali
katika biashara yao.
Hata hivyo kabla ya
msaada huo walijichangisha kiasi cha shilingili laki nane kwa kila
muhanga nakufanikiwa kukusanya shilingi milioni mia mbili iliyowasaidi
kuanza ujenzi wa soko hilo.
Aidha mwenyekiti huyo
ameomba taasisi nyingine ili kuweza kuwasaidia kuwapatia mitaji ili
kuweza kuanza upya tena biahsra hiyo ya uuzaji wa vinyago.
No comments:
Post a Comment