Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na watoto katika kituo cha New Life cha Boko.
Miss Tanzania Lilian Kamazima
(kulia) akimkabidhi zawadi ya mwaka mpya Msimamizi wa kituo cha kulelea
watoto yatima cha New Life kilichopo Boko, Mwanaisha Magambo kwa ajili
ya watoto 102 waliopo kituoni hapo, tukio hilo lilifanyika juzi.
Miss Tanzania Lilian Kamazima
(kushoto) akiwa na Miss Kinondoni Maria Shila wakiwa wamembeba mtoto
aliekuwa kwenye kituoo cha kulelea watoto yatima cha New Life cha Boko,
mtoto huyo alifikishwa hapo akiwa na siku nne tu tangia kuzaliwa kwake
………………………………………………………………………….
Redds Miss Tanzania 2014 Lilian
Deus Kamazima jumapili iliyopita alitoa misaada ya vyakula vya aina
mbalimbali kwa kituo cha New Life Orphans Home kilichopo eneo la Boko
nje kidogo ya jiji la D’salaam.
Kituo hicho ambacho kilianzishwa
mwaka 2005 awali kilikuwa maeneo ya magomeni makuti kilianza na watoto
yatima 17 na baadae kuongezeka hadi kufikia 70. Na kulazimika kuhama
eneo hilo na kuhamia kigogo ambapo waliishi eneo hilo hadi hivi karibuni
walipopata mfadhili mmoja kutoka nchini Qatar ambaye amewajengea jumba
moja kubwa na la kisasa eneo la Boko Dawasa, alisema bi Mwanaidi Magambo
ambaye ni Mlezi wa Kituo hicho.
Kituo hicho kina watoto wapatao
105 ambapo 60 kati yao ni wasichana na 45 wavulana. Kituo hicho kinalea
watoto wadogo kabisa wa umri wa mwezi mmoja hadi miaka 18. Hivi karibuni
tulimpokea mtoto mwenye umri wa siku 5 kutoka hospitali ya wilaya ya
Temeke ambaye mama yake alifariki mara tu baada ya kujifungua, alisema
bi. Magambo.
Kituo hicho kwa sasa kina matatizo
ya vyakula, vitanda, magodoro, madaftari pamoja na sare za shule kwa
ajili ya watoto hao yatima. Bi Magambo alimshukuru sana Mfadhili huyo
kutoka nchi ya Qatar kwa kuwajengea jengo hilo, lakini alisema kwa sasa
watahitaji mfadhili wa kuwalipia bili za umeme na maji pamoja na
mahitaji mengine kituoni hapo.
Kituo hicho kina bahati ya
kutembelea na warembo wa Miss Tanzania ambapo mwaka 2007, Miss Tanzania
2000 Jacqueline Ntuyabariwe alitembelea kituo hicho wakati bado wapo
eneo la Magomeni Makuti na kuwapatia misaada mbalimbali.
Miss Tanzania 201 4 Lilian
Kamazima alikabidhi vyakula vya aina mbalimbali ikiwemo mchele, unga wa
ngano, sembe, sukari, maharage, mafuta ya kupikia, sabuni, soda, juisi,
maji ya kunywa, na biskut vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni
mbili.
Miss Tanzania 2014 Lilian
aliishukuru kampuni ya Swissport Tanzania ambao ndio waliofadhili ziara
yake hiyo, na kuwaomba watanzania wengine kujitokeza kwa wingi kusaidia
watoto yatima na wengine wanaoishi katika mazingira magumu.
Ziara hiyo ya mrembo wa Taifa
Lilian ilikuwa ni zawadi ya sikukuu za mwisho wa mwaka ambao ililenga
kuwafariji watoto waliopoteza wazazi wao kwa namna moja au nyingine, na
pia kutimiza Kauli mbiu ya mashindano ya urembo ya Miss Tanzania isemayo
[Beauty with Purpose] Urembo na Malengo.
No comments:
Post a Comment