MFUKO wa Pensheni wa PSPF
umedhamini mchezo wa kirafiki utakaowakutanisha wachezaji waliowahi
kuwika katika timu kongwe nchini Simba na Yanga.
Mchezo huo unatarajiwa kufanyika tarehe 1 Januari 2015 katika
uwanja wa chuo cha Bandari, Tandika jijini Dar es Salaam, kiingilio
kitakuwa bure ikiwa ni zawadi ya mwaka mpya kutoka PSPF.
Katika mchezo huo baadhi ya wachezaji wa Simba wanaotarajiwa
kushuka uwanjani ni Thomas Kipese, George Lucas, Bita John, George
Masatu, Mustafa Hoza, Emmanuel Gabriel, Idd seleman. Timu ya Simba
inafanya mazoezi katika uwanja wa Leaders uliopo Kinondoni, ipo chini
kocha mchezaji Kasongo Athuman.
Wanaotarajiwa kushuka uwanjani kwa upande wa Yanga ni Peter
Manyika, Mwanamtwa Kihwelo, Edibily Lunyamila, Mohamed Husein, Chibe
Chibindu, Aboukar Salum, Bakari malima. Yanga wanafanya mazoezi katika
uwanja wa kauda ulipo katika makao makuu ya klabu hiyo kariakoo Jijini
Dar es Salaam, wakiongozwa na kocha Peter Tino.
Lengo la mchezo huo ni kutoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Dar
es Salaam na maeneo ya karibu hususani katika kipindi hiki cha sikukuu
za mwisho wa mwaka. PSPF itatumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mpya
ambazo Mkopo wa Elimu na Mkopo wa Kuanza Maisha. Tunatoa mwito kwa
wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwaona
wakongwe waliowahi kutikisha nchi katika anga ya soko nchini.
No comments:
Post a Comment