Maafisa
nchini Somali wanasema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa
Alshabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na
Somali.
Kamishna wa Wilaya ya El Wak mjini Gedo ameiambia BBC
Somalia kwamba vikosi vya usalama vilimkamata Zakariya Ismail Ahmed
Hersi katika maficho yake ndani ya nyumba moja baada ya kupashwa habari.
Mwaka 2012 Marekani ilitoa zawadi ya dola millioni 3 kwa yeyote yule ambaye angeweza kutoa habari za Hersi.
Kundi
la Al Shabaab limejiondoa kutoka miji kadhaa nchini Somalia tangu
uzinduzi wa mashambulizi makali dhidi ya kundi hilo yanayotekelezwa na
vikosi vya AMISOM vikishirikiana na wanajeshi wa serikali ya Somalia.
Bwana Hersi alikuwa kiongozi wa kundi la Alshabaab upande wa Amniyat.
Mapema
mwaka huu alikosana na kiongozi wa kundi hilo Ahmed Abdi Godane ambaye
aliuawa katika mashambulizi ya Marekani mnamo mwezi Septemba.
No comments:
Post a Comment