Mkurugenzi
wa Mboni Show, Mboni Masimba (wa pili ktoka kulia) akizungumza na
waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo
jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kuanza kwa msimu wa tatu wa
kipindi chake ‘The Mboni Show’ kinachotarajia kuanza Jan 2, 2015.
Kushoto ni kiti Simpompa na kuanzia kulia ni Afisa Masoko wa Mfuko wa
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira Werema na Kaimu Mkurugenzi wa
Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba.
Kutoka
Kulia Afisa Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) Magira
Werema akizungumza wakati wa uzinduzi kipindi cha Mboni Show uliofanyika
katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Pembeni ni
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC,Bw.Fadhili Chilumba pamoja na Mkurugenzi
wa Mboni Show, Mboni Masimba.
Na Mwandishi Wetu.
Mkurugenzi
wa Mboni Show, Mboni Masimba ameamua kuhamishia kipindi cha Mboni show
katika kituo cha utangazaji cha Taifa (TBC) kutoka EATV ili kuvutia
watazamaji wengi na wapya kwa wazee pamoja na vijana.
Kipindi cha Mboni Show kitaanza kurushwa TBC kuanzia January 2 mwaka 2015 siku ya
Ijumaa saa 3 Usiku-4 Usiku na marudio Jumanne saa 9:00 mchana-10:00mchana.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana jijini Dar ndani ya ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Mboni Masimba ametoa shukrani kwa EATV kwa ushirikiano
wao kwa kipindi chote alichokuwa nao,na kusema kuwa amehamishia kipindi
cha Mboni Show katika kituo cha TBC ili kuvutia watazamaji wengi hakuna
atakaye tumia jina la Mboni Show na hakuna kitakachomkwamisha kwa vile
ana hati miliki.
“Nimeamia
TBC kwa kuwa nahitaji watazamaji wengi ,wote wazee na vijana na hakuna
atakaye tumia jina langu la Mboni Show kwa kuwa nina hati miliki ya jina
hili”alisema Mboni.
Kwa
upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Masoko TBC, Bw.Fadhili Chilumba amesema
wamefurahi kuwepo kwa Mboni Show katika kituo cha Taifa(TBC) na kutoa
wito kwa mashabiki kuweza kuwadhamini watu kama wakina Mboni na
wanamkaribisha sana.
Nao
wadhamini wa Mboni Show,Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (PSPF)
Magira Werema wamesema wanamwezesha Mboni kuwepo hewani ili
kuhamasisha,kuelimisha pamoja na kuburudisha umma wa Watanzania.
No comments:
Post a Comment