WENCE AKITOA ELIMU KWA WANAHABARI WALIOKUTANA MKOANI IRINGA
WANAHABARI NWAKIWA MAKINI KUMSIKILIZA MTOA ELIMU
…………………………………………………………………………….
Waandishi wa habari wametakiwa
kuandika zaidi habari zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia hususan dhidi
ya wanawake na watoto ili kuiamsha zaidi jamii inayowafanyiwa vitendo
hivyo na mamlaka husika ziweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
vitendo hivyo.
Msisitizo huo ulitolewa na chama
cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa waandishi wa
habari wa mikoa ya nyanda za juu kusini (IRINGA,MBEYA,UVUMA NA NJOMBE)
ambapo wanahabari wameombwa kuendelea kufichua habari hizo hususan kwa
wanaofanyiwa vitendo hivyo ili waweze kuelewa kwamba sheria dhidi ya
ukatili huo zipo na kwamba kuna taasisi za kuwatetea.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mwanahabari wa siku nyingi
WENCE MUSHI alisema dhahiri kuwa vitendo vya unanyanyasaji vimepungua
kutokana na wanaofanya ukatili huo kuelewa, na watendewa pia kuzidi
kuamka, juhudi zaidi zilitakiwa kujipenyeza zaidi dhidi ya imani za
kimila ambazo bado zinashikiliwa katika sehemu mbalimbali za nchi.
“Endeleeni kutumia kalamu zenu na
vifaa vyenu vyote kupiga vita vitendo vyote vinavyotokana na manyanyaso
ya kijinsia ambayo hasa hutokana na mfumo dume,” alisema wence akiwaomba
wahabari kufanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza juhudi za kutokomeza
kabisa suala la unyanyasaji wa kijinsia.
Wence alisema jicho la waandishi
wa habari linasaidia kuwaelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali
yanafanywa kinyume cha seria,kuwaomba wanahabari kufanya habari za
kichunguzi juu ya ukatili wa kijinsia pamoja na unyanyasaji wake.
Pia aliongeza kwa kusema kuwa kwa
sasa TAMWA imekijita katika kufuatilia habari juu ya ukatili wa kijinsia
pamoja na mauwaji ya watu wenye ulemavu na kulenga hasa habari za
kichunguzi ambazo zitaleta mabadiliko kwa jamii yetu.
Kwa upande wa waandishi wa habari
wa nyanda za juu kusini walioshiriki warsha hiyo wamesema kuwa wanafanya
kazi hiyo katika mazingira magumu,hivyo kuwaomba TAMWA kuwasaidia
chombo cha usafiri kila mkoa ili waweze kuwafikia wananchi waliopo
vijijini na kupata taarifa zao.
Lakini wakawataka wanahabri
wengine kufanya kazi kwa kufuta weledi wao kutokana na elimu walioipata
wakiwa darasa na kwenye mafunzo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment