Kamati
ya Utendaji ya Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini -TFF iliyokutana
jumapili Februari 22 mwaka huu, imefanya mabadiliko ya mahali
utakaofanyika Mkutano Mkuu wa mwaka kutoka Mkoa wa Sinigida na
kuhamishia mkoa wa Morogoro.
Hatua hiyo imefikiwa na Kamati ya
Utendaji kutokana na sababu za kutokukamilika kwa miundombinu ya mkutano
mkuu na kuwepo ka shughuli nyingine za kijamii mkoani humo.
Kamati ya Utendaji inamshukuru
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Singida (SIREFA), na
uongozi mzima kwa kujitolea kuandaa mkutano huo na huko nyuma waliweza
kuandaa mkutano wa makatibu wa vyama vya soka vya mikoa.
TFF itaandaa vikao na matukio
mengine mkoani Singida itakapotokea hapo baadae, tarehe ya mkutano mkuu
itaendelea kubakia ile ile ya Machi 14, 15 mwaka huu.
NASRY KUJIUNGA NA ASPIRE FOOTBALL DREAM SENEGAL
Kijana Nasry Daudi Aziz
aliyezaliwa Agosti 21, 2001 amechaguliwa kujiunga na kituo cha kukuza
vipaji cha Aspire Football Dream kilichopo katika mji wa Dakar nchini
Senegal.
Mradi wa Aspire nchini ulianza
mchakato wa kusaka vijana mwezi Machi – Mei, 2014 ambapo vijana wengi
walijitokeza na kuchaguliwa vijana 14 ambao walikwenda katika mchujo
mwingine uliofanyika nchini Uganda uliowashirikisha vijana zaidi ya 50.
Kijana huyo ni miongoni mwa
wachezaji 17 waliochaguliwa kati ya vijana 34 walikuwepo nchini Senegal
kwa muda wa mwezi mmoja, ambapo kulikuwa na vijana wengi kutoka nchi
mbalimbali barani Afrika na Amerika ya Kusini.
Kituo cha Aspire kilichopo Dakar
nchini Senegal ni miongoni mwa vituo viwili vinavyoongozwa na mtoto wa
mfalme wa Qatar na timu ya Barcelona, kituo kingine kipo mjini Doha.
Nasry Daud Aziz anatarajiwa
kuondoka nchini Februari 28 mwaka huu kuelekea Dakar ambapo atakua
kwenye kituo hicho kwa mkataba wa miaka miatano.
Kutoka nchini Tanzania Nasry
anakua ni kijana wa tatu kujiunga na kituo hicho, wengine ni Matine
Taganzi na Orgenes Morrel ambaye aliitwa kwenye timu ya Taifa Stars
maboresho na kocha Mart Nooj.
STAND NA SIMBA ZAINGIZA MIL 31, MBEYA CITY, YANGA MIL 74
Mchezo uliokuwatanisha wenyeji
timu ya Stand United kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga dhidi ya
timu ya Simba umeingiza jumla ya tsh. milioni 31.
Juma la watazamaji 5,439 waliingia
uwanjani kushuhudia mchezo huo, ambao timu ya Stand imepata mgao wa
tsh. 6,564,268.22 na Simba wakipata mgao wa tsh. 4,661,581.78.
VAT (18%) tshs. 4,763,135.59 huku
FA mkoa wakipata tsh.665,940.25, FDF tsh. 1,141,611.86, Bodi ya Ligi
tsh. 1,522,149.15, Gharama za mchezo tsh. 1,617,283.47, Uwanja tsh.
2,854,029.66, Gharama ya tiketi tsh. 1,593,000,00, FDF tsh.
2,921,000.00, TFF tsh.2,921,000.00
Katika uwanja wa Sokoine mbeya
jumla ya tsh. 74,600.000.00, zilipatikana kutokana na watazamaji 14,920
waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo, VAT(18%) tsh.11,379,661.02,
CDRB (5%) tsh.3,730.000.00, FDF tsh. 5,222,000,00, TFF tsh.
2,238,000.00, Uwanja tsh. 7,804,550,85, Gharama za mchezo tsh
4,442,578.81, Bodi ya Ligi tsh. 4,162,427,12.
Chama cha soka mkoa (FA) Mbeya
kimepata tsh. 1,821,061.86, FDF(TFF) tsh. 3,121,820.34, wenyeji timu ya
Mbeya city wakipata tsh. 17,950,466.95 na klabu ya Yanga tsh.
12,747,438.98.
No comments:
Post a Comment