Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es salaam wakati alipotangaza kuhusu malipo
mbalimbali yaliyotolewa kwa vituo vya watoto yatima kwa ajili ya kulipia
karo za wanafunzi wanaosoma katika shule mbalimbali nchini, Msama
ameyasema hayo wakati akizunguzia maandalizi ya sherehe zakutimiza miaka
15 kwa Tamasha la Pasaka zinazotarajiwa kufanyika Aprili 7 mwaka huu
jijini Dar es salaam na kushirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa
injili kutoka Tanzania na mataifa mbalimbali Kusini mwa Afrika, Ukanda
wa Maziwa Makuu na Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Ulaya kutoka
kule nchini Uingereza wanaotarajiwa kutoa burudani katika tamasha hilo
litakaloshirikisha michezo mbalimbali pia, Kushoto ni Bw. Khamis Pembe
mmoja wa waratibu wa tamasha hilo.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akisisitia jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakichukua taarifa na taswira za picha wakati wa mkutano huo.
No comments:
Post a Comment