TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Saturday, February 28, 2015

MTEJA WA BENKI YA AFRIKA TANZANIA (BOA) ASHINDA GARI LA KISASA

Gari aina ya Toyota Brevis lililotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya Droo ya mwisho ya Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana.
 
Meneja Uendeshaji Biashara wa Benki ya Afrika Tanzania (BOA), Bw. Wasia Mushi akiwaonyesha waandishi wa habari gari mpya aina ya Toyota BREVIS lililotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya Droo ya mwisho ya Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana. Wengine ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Bw. Emanuel Moya (kulia) na Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Mirisho Millao.

Baadhi ya waandishi wa habari walioshuhudia Promosheni hiyo,

Meneja Uendeshaji Biashara wa Benki ya Afrika Tanzania (BOA), Bw. Wasia Mushi (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu droo ya mwisho ya Pormosheni ya ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana. Kulia ni Meneja wa Benki hiyo Tawi la Kijitonyama, Bw. Emanuel Moya na Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Bw. Mirisho Millao.

Mteja wa Benki ya Afrika Tanzania (BANK OF AAFRIKA TANZANIA BOA), Bw. Ismail Said Mohamed, wa Tawi la Benki hiyo  mkoani Mtwara, ametangazwa leo kuwa mshindi gari mpya aina ya TOYOTA BREVIS, wakati wa droo ya mwisho ya Promosheni ya Deposit and Win iliyoanza Oktoba mwaka jana.

Wakati Bw. Mohamaed akishinda gari hilo mpya, mteja mwingine Thureiya Zabron Mgamba ameibuka mshindi wa pili wa Promosheni hiyo iliyofanyika kwenye tawi la Benki hiyo Kijitonyama baada ya kushinda Pikipiki mpya aina ya TOYO.

Katika mchezo huo wa Bahati Nasibu uliosimamiwa na Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha, Bw. Mrisho Millao, washindi wengine watatu pia walishinda zawadi mbalimbali zikiwemo Tshirt, Simu za kisasa na vocha za manunuzi.

Awali akizungumza na waanndishi wa habari, kabla ya Promosheni hiyo, Meneja Uendeshaji Biashara wa BOA, Bw. Wasia Mushi, amesema, lengo la Poromosheni hiyo ni kuongeza hamasa kwa watanzania ili wakumbuke kujiwekea akiba, huku akisisitiza kuwa kujiwekea akiba ndio utamaduni halisi wa kuelekea katika mafanikio.

Bw. Mushi amesema wakati wote wa Promosheni hiyo iliyofanyika nchi nzima, wateja zaidi ya 2000 wa Benki hiyo walishiriki na kushinda zawadi mbalimbali. “Tumefurahishwa sana jinsi Promosheni hii ilivyopokelewa na wateja wetu, tumeongeza idadi ya wateja pia kukuza amana kwa wateja wetu”, anasema Bw. Wasia.

Amesema pamoja na Promosheni hiyo kufikia tamati, Benki ya Afrika bado inaendelea kuwahimiza wateja kuweka akiba kwa ajili ya manufaa ya jamii na kuahidi kuwa wamejipanga kutoa huduma za kisasa kwa wateja.

Bw. Wasia amesema Benki ya Afrika Tanzania imejiikuwa ikijimalisha kwa kuwa na mtandao wa matawi 20 nchi nzima, ambapo matawi kumi yako Jijini Dar es Salaam, wakati matawi mengine yakiwa Arusha, Kilimanjaro, Mwanza, Morogoro, Mtibwa, Kahama, Mbeya, Mtwara na Tunduma.

No comments:

Post a Comment