Mkurugenzi
wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Ally Mohamed akionyesha moja ya
chapisho lenye taarifa za tafiti za watu walio katika makundi maalum na hali ya maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi katika mikoa 7 lililotambulishwa
leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho (kushoto) chapisho lenye taarifa za utafiti kwa watu walio katika makundi maalum na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mikoa 7 leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akimkabidhi Meneja Mpango wa Tume ya Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) Dkt. Robert Josiah (kushoto) chapisho lenye taarifa za utafiti kwa watu walio katika makundi maalum na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mikoa 7 leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Udhibiti na Uhakiki wa Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Ally Mohamed (katikati) akiwa ameshika chapisho lenye taarifa za utafiti kwa watu walio katika makundi maalum na hali ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mikoa 7 akiwa na baadhi ya watendaji wanaoongoza taasisi za kupambana na Ukimwi nchini .

Picha ya
pamoja ya washiriki hao baada ya uzinduzi wa chapisho.
Na. Aron Msigwa –
MAELEZO.
23/2/2015. Dar es
salaam.
SERIKALI imesema kuwa
itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya kutoa elimu kwa makundi
ya watu wanaotumia dawa za kulevya na wale wanaojihusisha na biashara ya ngono
katika maeneo mbalimbali nchini ili
kukabiliana na maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi .
Akizungumza kwa niaba
ya Mganga Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Udhibiti na
Usalama wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.Mohamed Ally Mohamed wakati wa
kutambulisha matokeo ya tafiti za watu walio katika makundi maalum yaliyo
katika hatari ya kuambukizwa Virusi vya
Ukimwi katika mikoa 7 iliyofanyiwa
utafiti ambayo ni Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Iringa, Mara, Tabora na
Shinyanga.
Akitambulisha matokeo
hayo Dkt. Mohamed amesema kuwa hali ya maambukizi mapya miongoni mwa wanaume na wanawake katika maeneo
yaliyofanyiwa utafiti imekuwa ikipungua kwa kasi ndogo licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali kwa na wadau
mbalimbali kukabiliana na maambukizi hayo kutokana na makundi hayo kutobadili
tabia.
Amesema maeneo
mbalimbali yaliyofanyiwa utafiti na wataalam wa Wizara ya Afya, taasisi za
kitaifa na Kimataifa zinazojihusisha na Ukimwi yameonesha uwepo wa tabia
hatarishi zinazochangia maabukizi mapya ya VVU yakihusisha makundi watu walio katika makundi maalum ya
wanawake wanaofanya biashara ya ngono, wanaume wanaofanya ngono ya jinsia moja
pamoja na watu wanaojidunga dawa za kulevya.
Amefafanua kuwa katika
mikoa 7 ambayo imefanyiwa utafiti huo hali ya maambukizi ya VVU kwa wanawake
imeonekana kuwa kubwa pamoja na ongezeko la wanaume wanaofanya ngono na wanaume
wenzao huku idadi ya wanaojidunga dawa za kulevya ikikadiriwa kuwa kati ya
7,000 hadi 10,000.
“Hali ya maambukizi
katika mikoa ulikofanyika utafiti ni kubwa, wanawake wana maambukizi
makubwa, idadi ya wanaojidunga dawa za
kulevya inakadiriwa kuwa kati ya 7,000 hadi 10,000 huku kiwango chao cha
maabukizi ya VVU kwa asilimia kikiwa asilimia 15.5 kiwango hiki ni kikubwa”
Amesema Dkt. Mohamed.
Kwa upande wake Meneja Mpango wa Tume ya Taifa wa Kudhibiti Ukimwi
(NACP) Dkt. Robert Josiah akizungumzia kuhusu tafiti hizo amesema kuwa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za taifa na
kimataifa ilifanya tafiti tatu za makundi yaliyo katika hatari ya kuambukizwa
VVU ili kubaini makisio ya idadi ya watu walio katika makundi hayo.
Dkt.Robert ameeleza kuwa tafiti hizo zilifanyika katika vipindi
tofauti kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 kwenye mikoa yenye viwango vya juu vya
maabukizi ya VVU na kueleza kuwa mkoa wa Iringi unaongoza kwa kuwa na asilimia
9.1, ukifuatiwa na Mbeya 9.0%, Shinyanga 7.4%, Dar es salaam 6.9%, Tabora 5.1%,
Mara 4.5% na Mwanza 4.2.
Amesema kwa kutumia
matokeo hayo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweza kubaini changamoto
mbalimbali na hali ya maambukizi ya VVU miongoni mwa makundi ya watu walio
katika makundi hatarishi kwa lengo la kubaini mbinu mbalimbali za kutoa huduma
za kinga, tiba na matunzo kwa watu walio katika makundi hayo.
“Kwa upande wetu
tutatumia takwimu hizi kuboresha huduma ztu na kupanga mipango mbalimbali ya kupunguza
maambukizi ya Ukimwi nchini, lengo la NACP ni kuhakikisha kuwa Tanzania
inaondokana na maambukizi ya VVU” Amesema.
Naye Mwenyekiti
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho
akizungumzia matokeo ya tafiti hizo amesema kuwa ipo haja ya tafiti
zinazofanyika nchini kuendelea kutazama jinsia zote ili kupata uhalisia katika
jamii kwa makundi maalum.
Ametoa wito kwa
Serikali na wadau mbalimbali kuzitumia takwimu zilizopatikana ili kufanya
mabadiliko ya mbinu na njia za kukabiliana na maambukizi mapya ya VVU nchini
Tanzania.
No comments:
Post a Comment