WATU
WATATU KATI YAO MWANAUME MMOJA UMRI KATI YA MIAKA 45 – 50, MWANAMKE
MMOJA UMRI KATI YA MIAKA 65 – 70 NA MTOTO WA KIKE UMRI KATI YA MIAKA 10 –
12 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.144
CGX/T.569 CKC AINA YA FAW TRACK LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA KUYAGONGA MAGARI MATATU AMBAYO NI T.158 BSJ AINA YA TOYOTA
PICK-UP LIKIENDESHWA NA EMANUEL SHEDAFA (28) MKAZI WA MWAKIBETE, GARI
T.584 DRB AINA YA TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DENIS VICTOR (27) MKAZI
WA NZOVWE NA GARI T.623 ADQ AINA YA TOYOTA HIACE LIKIENDESHWA NA DEREVA
ASIYEFAHAMIKA AMBALO LILIPOTEZA UELEKEO NA KUTUMBUKIA MTONI NA
KUSABABISHA VIFO.
AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE
22.02.2015 MAJIRA YA SAA 16:45 JIONI HUKO ENEO LA MLIMA MBALIZI, KATA YA
SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA
KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUNDUMA. AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU 14
WALIJERUHIWA KATI YAO 13 WAMELAZWA HOSPITALI TEULE YA IFISI NA MMOJA
AMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATI YA MAJERUHI HAO 04 NI
WANAWAKE NA 10 NI WANAUME. CHANZO CHA AJALI BADO HAKIJAFAHAMIKA. DEREVA
WA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. NA T.144 CGX/T.569 CKC AINA YA FAW
TRACK ALIKIMBIA NA KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA
ZINAENDELEA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WAHAMIAJI HARAMU WAWILI
WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. SIFA BUKULU (35) NA 2. NYOTA RAMADHANI
(30) PAMOJA NA WATOTO WADOGO WATATU WOTE RAIA NA WAKAZI WA SANGE NCHINI
KONGO WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WAHAMIAJI HAO WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 22.02.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO ENEO LA MAJENGO, KATA
NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA
KUWAFIKISHA IDARA YA UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. AMANI MBEGA
(43) MKAZI WA MOSHI NA 2. HAKIMU WATSON (40) MKAZI WA MAJENGO WAKIWA NA
SILAHA BUNDUKI AINA YA SHOTGUN ILIYOTENGENEZWA KIENYEJI NA RISASI MOJA.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 22.02.2015 MAJIRA YA SAA 22:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA
ITUMBA, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA KIPOLISI MBALIZI, MKOA WA MBEYA
BAADA YA KUFANYIKA MSAKO. SILAHA HIYO ILIKUWA IMEFICHWA KWENYE DARI LA
NYUMBA YAO.
KATIKA MSAKO WA TATU, WATU WAWILI
WOTE WAKAZI WA MPEMBA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. LUCAS KAYUNI (28)
NA 2. MANENO KAYUNI (20) WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
WAKIWA NA MICHE 10 YA BHANGI IKIWA IMEPANDWA KWENYE SHAMBA.
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO
TAREHE 22.02.2015 MAJIRA YA SAA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA
MPEMBA, KATA YA CHIWEZI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA
MBEYA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII WANANCHI NA KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO DEREVA
ALIKIMBIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment