WAZIRI WA NISHATI NA MADINI MHE. GEORGE SIMBACHAWENE AKABIDHIWA RIPOTI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI KWA MAKAMPUNI YA UZIDUAJI NCHINI
Kaimu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava
(kulia) akimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Mhe. George
Simbachawene (kushoto) ili aweze kuzungumza na timu ya majaji na
sekretarieti iliyofanya kazi ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya
Utoaji wa Huduma za Jamii na Uwezeshaji kwa makampuni ya uziduaji yaani
madini na gesi. Timu hiyo iliendesha zoezi hilo mapema Septemba, mwaka
jana.
Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene akielezea umuhimu wa
kuhamasisha makampuni mengi zaidi kujitokeza katika kuwania tuzo ya
Rais katika utoaji wa huduma kwa jamii na uwezeshaji kwa makampuni ya
gesi, mafuta na madini ili wananchi wafaidike zaidi na mchango katika
sekta za nishati, madini na gesi.
Waziri
wa Nishati na Madini Mhe. George Simbachawene (aliyekaa mbele)
akizungumza na timu ya majaji na sekretarieti iliyofanya kazi ya
kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Utoaji wa Huduma za Jamii na
Uwezeshaji kwa makampuni ya uziduaji yaani madini na gesi.
No comments:
Post a Comment