Zipo taarifa za kutokea kwa vurugu kubwa katika eneo la
Ilula mkoani Iringa.Taarifa zinadai kuwa vurugu hizo ni kati ya jeshi la
polisi na wananchi wa kawaida ambao wamefunga barabara kwa kuwasha moto
wa matairi ya gari.
Aidha taarifa kutoka kwenye eneo la tukio zinaendelea
kueleza kuwa hadi sasa magari manne ya Polisi na Pikipiki moja
vimechomwa moto, huku basi linalofahamika kwa jina la Nyagawa
linalosafirisha abiria kutoka Njombe kuja Dar es Salaam likiwa
limevinjwa vioo vyote.
Taarifa hizo zinadai kuwa tayari polisi wa kutuliza ghasia
FFU wameshafika eneo la tukio na kufanikiwa kwa sehemu kutuliza ghasia
hizo, na kwamba magari yanayokuja Dar es Salaam na mikoa mingine
yameshaanza safari zake.
Ungana nasi baadaye kwa taarifa zaidi
Chanzo Mwananchi
…………………………………
PICHA KWA HISANI YA IRINGA YETU BLOG
No comments:
Post a Comment