Benki ya
Posta Tanzania (TPB) na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wamekabidhiana
rasmi mradi wa huduma kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Tanzania Postal Bank (TPB) and Tanzania Telecommunications Company Ltd (TTCL) haveLengo la
mradi huu ni kuhakikisha kuwa TPB inatanua wigo wa utoaji huduma zake
kwa ufanisi na tija kwa kupitia huduma hii kutoka TTCL. Huduma hii
inayopatikana kupitia katika Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano una faida
ambazo toka mradi huu ukamilike Benki ya Posta Tanzani (TPB) imefaidika
ikiwa ni pamoja na kupungua kwa muda wa wateja
kusubiria huduma kwenye matawi , kuongezeka kwa ufanisi wa utendaji
kazi wa ndani ya benki, kulinda taarifa za wateja na kampuni kwa
ujumla.
Makao Makuu
na matawi Kumi (10) ya Benki ya Posta Tanzania (TPB) yameunganishwa
kwenye mtandao wa TTCL wa MPLS-VPN kupitia kwenye Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano, ambao umeongeza wigo wa utoaji wa huduma zilizo bora kwa
wananchi walio vijijini na mjini nchi nzima.
Matawi hayo
ambayo yameunganishwa katika Mtandao wa TTCL,ni pamoja na Makao makuu
ya TPB, Ofisi za Dar es Salaam, Samora, Kijitonyama, Sam Nujoma na
Ubungo. Matawi mengine ni YWCA, Metropolitan, Arusha, Dodoma, Mbeya na Mwanza.
Kwa kutambua
mageuzi na uhitaji wa teknolojia katika kutoa huduma, Benki ya Posta
Tanzania (TPB) iliamua kutekeleza mradi huu kwa lengo la kuongeza
ufanisi na tija katika kutoa huduma kwa wateja wake ambao wameenea
katika mikoa na wilaya nchini kote.
Benki ya
Posta Tanzania ni benki inayomilikiwa na Serikali kwa asilimia kubwa,
itaendelea kuunganisha matawi yake nchi nzima, yale ya mikoa na wilaya
ili kuwafikia watanzania waliowengi wenye mahitaji ya huduma za kibenki.
Benki ya
Posta Tanzania (TPB) tunajivunia kuwa benki pekee yenye ofisi mpaka
ngazi ya wilaya, yenye kutumia teknolojia ya kisasa, za haraka na nafuu
katika kutoa huduma kwa wateja wake.
Tunapenda kuweka wazi kuwa kwa kutumia huduma hii ya Mult- Protocol Label Switching -Virtual Private Network (MPLS –VPN), taarifa za benki na wateja wake zitakuwa salama zaidi.
Pia, TPB
inatarajia kuanza kutekeleza awamu ya pili ya kuunganisha matawi yake
28 nchi nzima kwenye Mtandao wa TTCL, wa MPLS VPN ambao unapitia katika
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ikiwa ni dhumuni la dhati la kuongeza
tija katika kutoa huduma.
No comments:
Post a Comment