Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Ibrahim Msengi Akizindua Nakala
ya Katiba Pendekezwa ili ziweze kugawiwa kwa Mkoa wa Katavi,kushoto kwa
Mkuu wa Mkoa Ni Katibu Tawala wa Mkoa Mhandisi Emanuel Kalobelo pamoja
na Viongozi wengine wa Mkoa huo.
Mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Mlele
Wilbroad Mayala akipokea Nakala ya Katiba kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dkt Ibrahimu Hamis Msengi kwa niaba ya Mkurugenzi ili
vikagawiwekwa kwa wananchi wa Halmashauri yake waweze kuvisoma.
…………………………………………………………………
Na Kibada Ernest-Katavi.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt
Ibrahimu Hamisi Msengi amewaasa wakazi wa Mkoa huo kujenga utamaduni wa
kusoma nyaraka mbalimbali ili kujijengea uelewa wa mambo muhimu, na
amewasisitiza wananchi wa Mkoa huo kusoma nakala za Katiba
inayopendekezwa ili siku itakapofika ya kwenda kuipingia kura wawe na
umaamuzi sahihi.
Dkt Msengi ametoa Rai hiyo
wakati wa kikao kati yake na Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa,
Wataalamu wa Kada mbalimbali, Taasisi za Serikali zilizopo katika Mkoa
huo,Kamati za ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa, Watendaji wa
Mitaa,Wazee Mashuhuri na Viongozi wa Madhehebu ya dini kilichofanyika
jana(juzi)kwenye ukumbi wa Mikutano Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Kikao hicho kilichoambatana na uzindua wa Nakala za Katiba pendekezwa zilizoletwa Mkoani Katavi ili ziweze kugawiwa kwa wananchi waweze kuzisoma na kuzielewa kabla zoezi la kuipigia kura Katiba pendekezwa muda utakapofika.
Amesema watanzania wamekuwa na
tabia ya kutopenda kusoma nyaraka muhimu hivyo kuwa na tabia ya kudharau
mambo ambapo nyaraka hizo ni muhimu kama Katiba inayopendekezwa iwapo
wataisoma wataweza kuelewa kwa undani kilichoandikwa na watakapokwenda
kupiga kura watakuwa na uamuzi wa kufanya, kwa kuwa watakuwa wanafahamu
kile kilichoandikwa ndani ya Katiba pendekezwa.pia unaweza kuisoma
ukaelewa na ukashindwa kutoa maamuzi.
“Tuondokane na ugonjwa huu wa
kutokusoma tuwe na tabia ya kujisomea ili tuwe na uhakika wa mambo
tunayoyafanya”amesema Dkt Msengi.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa rai
kwa wakazi wote wa Mkoa huo kujenga tabia ya kusoma nyaraka, na waisome
Nakala ya katiba iliyopendekezwa na kuielewa na muda ukifika wa kupiga
kura wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura ili watumie haki yao ya
kidemokrasia.
Akaongeza kuwa ili uwe na fursa
ya kupiga kura lazima ujiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga
kura.ili uweze kupiga kura kwa mjibu wa sheria lazima ujiandikishe.
Wakati ukifika wa kuboresha
daftari la kudumu la wapiga kura wananchi wajitokeze kwenda
kujiandikisha na wale ambao hawataweza kujiandikisha watakosa fursa
hiyo ya kidemokrasia ya kuipigia kura Katiba pendekezwa na kuwachagua
viongozi wao ambao ni Madiwani Wabunge na Rais katika uchaguzi Mkuu
utakapofanyika Oktoba mwaka huo.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa
Katavi Mhandisi Emanuel Kalobelo ameeleza kuwa Mkoa wa Katavi umepokea
jumla ya Nakala 15,640,za Katiba Pendekezwa kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ili ziweze kugawiwa kulingana na maelekezo ya ugawaji wa nakala
za katiba hizo.
Mhandisi Kalobelo ameeleza kuwa
mgao wa Nakala hizo umegawanywa kwa mpangilio kama ilivyoelekezwa kuwa
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda iligawiwa nakala 3,900,Halmshauri ya
Nsimbo Nakala 3,600,Halmashauri ya Mji Mpanda Nakala 3,600,Halmashauri
ya Wilaya ya Mlele Nakala 4,500, na wamekabidhiwa Wakurugenzi wa
Halmashauri za Mkoa.ambapo kwa upande wa Mkoa na taasisizilizopo katika
mkoa huo ulipokea nakala 40 kwa ajili ya kuzigawa kwenye Taasisi
zilizopo katika Mkoa huo.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda
Paza Mwamlima akimkaribisha Mkuu wa Mkoa amewaeleza Viongozi wote kuwa
wanatakiwa kufikisha ujumbe kwa wananchi wao na wawahamasishe wajitokeze
kwa wingi katika zoezi la kujianadikisha katika daftari la kudumu la
wapiga kura.
Pia amewasisistiza wapeleke
nakala hizo kwa wananchi wazisome ili waweze kuwa na uamuzi wa kuipigia
kura Katiba pendekezwa wakiwa na uelewa kuhusu Katiba hiyo Pendekezwa.
Kwa upande wake Katibu Tawala
Msaidizi ambaye pia ni Afisa Tawala wa Mkoa wa Katavi Salum Shilingi
akawaasa Viongozi hao kuwa ni Nakala hizo haziuzwi zinagawiwa bure,na
lengo lake ni kuwagawia bure wananchi wazisome ,atakayepatikana akiziuza
hatua kali zitachukuliwa juu yake.
Katika Hatua nyingine akapongeza
Gazeti la Mpandaleo kwa kueleimisha Jamii ya Mkoa wa Katavi na Mikoa
jirani kutokana na habari zake zinazoandikwa humu akasisitiza wananchi
waendelee kulisoma kwa kuwa ni kioo na kielelezo cha Mkoa.
No comments:
Post a Comment