Balozi
wa Canada nchini Tanzania, Mh. Alexandre Lévêque akimkabidhi tuzo ya
kwanza Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake
Tanzania-TAMWA,Bi. Valerie Msoka kwa kufanikisha kampeni dhidi ya ndoa
za utotoni.(Picha zote kwa hisani ya mtandao wa hivisasa.co.tz).
Mkurugenzi
wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania (TAMWA) Valerie Msoka,
amekuwa mtu wa kwanza kutunukiwa tuzo ya CEFM Champion, na Ubalozi wa
Canada nchini.
Katika
sherehe fupi iliyofanyika Serena Hotel 24 Februari 2015, Balozi wa
Canada nchini Bwana Alexandre Leveque alisema kuwa Valerie Msoka amekuwa
mwanaharakati wa kwanza kutunikiwa tuzo hiyo na ubalozi wake kama
ishara ya kukubali mchango wake kupiga vita ndoa za utotoni, za
kulazimishwa na ukeketaji kwa watoto wa kike nchini.
“Watoto
wa kike na wanawake wamevumilia machungu ya ndoa za utotoni na za
kulazimishwa hivyo wanahitaji mtu wa kuwasemea: mtu ambae ataelezea
taarifa zao zinakazosaidia kuwaweka watu pamoja na kuleta mabadiliko
yenye tija,”amesema Balozi Lévêque. Valerie Msoka atakuwa mtetezi.
Ninafuraha kumtangaza kuwa Mtetezi wa CEFM wa Ubalozi wa Canada nchini
Tanzania.”
Valerie
ametumia ujuzi wake kama mwanahabari aliyebobea, mwanaharakati na
mpenda maendeleo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali bila kujali
litakalomtokea au kueleweka vibaya na jamii.
Ameandika
taarifa zenye kuvuta hisia, huruma na kuhamasisha kasi ya mabadiliko
Katika jamii na watunga sera,” alisema Balozi Leveque.
Wapili
kutoka kushoto ni Balozi wa Canada nchini Tanzania Alexandre Lévêque ,
Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA Valerie Msoka, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Anna Maembe na wawakilishi
mbalimbali kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa wa masuala ya wanawake,
UNFPA na UN Women.
Watoto
wa kike milioni 14 duniani huozeshwa kila siku katika umri mdogo chini
ya 18 jambo ambalo ni kinyume cha haki za mtoto na ukiukwaji wa haki za
binadamu. Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa ndoa za utotoni
na mikoa husika ni Shinyanga, Tabora, Mara, Lindi, Mbeya na Morogoro.
Balozi
Leveque ameahidi kuunga mkono jitihada zinazomlinda mtoto wa kike ili
kuendeleza kampeni ya Zero Marriage kwa mkoa wa Mara iliyozindiliwa
mwaka 2014 na aliyekuwa mke wa Hayati Rais wa Kizalendo wa Afrika ya
Kusini Nelson Mandela, Graca Machel.
Akitoa
shukrani baada ya kupokea tuzo hiyo, Valerie Msoka alisema kuwa ndoa za
utotoni za kulazimishwa na ukeketaji vyote vinaenda pamoja na ni wajibu
wa wadau mbalimbali ikiwemo serikali na vyombo vya habari kuendeleza
kutoa elimu, kufanya tafiti ili kuwa na rekodi inayofahamika kuhusu
ukubwa wa tatizo, kufuatilia mwenendo na mafanikio ya kampeni mbalimbali
na kuendeleza hamasa kwa jamii kwa nini ndoa za utotoni zikomeshwe.
“Tukitaka
kufanikisha kampeni hii ni lazima tufanye kazi kwa pamoja na kwa moyo
mmoja, kuelewa nani anafanya nini kwa kiwango gani. Serikali nayo bado
tunaitegemea sana kwa hali na mali katika kubadilisha sera
zinazomkandamiza mtoto wa kike kwa kuzingatia mabadiliko ya katiba
mpya”, alisema Valerie.
Wadau
mbambali wa masula ya wanawake na waandishi wa habari wakongwe
(Ma-Veterans), kutoka kushoto ni Fatuma Aloo pamoja na Mama Rose Haji
Mwalimu wakihsuhudia tukio hilo.
“Tuzo
hii ni yetu wote, kama sio kwa ushirikiano wenu wadau wa maendeleo,
vyombo vya habari ambavyo tumefanya kazi kwa karibu sana na jamii kwa
ujumla. Ni matumaini yangu kuwa tutaendelea kushikamana kuhakikisha kuwa
hadhi ya mtoto wa kike inalindwa ipasavyo”.
Hii
ni mara ya pili kwa kiongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari Tanzania
(TAMWA) kupata tuzo ya kutambulika. Mwaka 2010 Ubalozi wa Marekani
ulimtunuku Mkurugenzi aliyemaliza muda wake Ananilea Nkya tuzo ya
Mwanamke Jasiri kutokana na mchango wake wa kuendeleza usawa, fursa na
haki kwa wanawake wa wasichana wa Kitanzania.
Akitoa
nasaha zake kwa niaba ya serikali, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya
Jamii, Watoto na Jinsia Bi Anna Maembe amempongeza Msoka kwa kazi nzuri
na chama anachokiendesha kwa ujumla na kusema kwamba tuzo hii imetolewa
wakati ambapo dunia na taifa kwa ujumla linatafakari matokeo ya Beijing
+20 ambako Katika maazimio 20 yaliyoainishwa, Tanzania ilipendekeza
kulifanyia kazi azimio moja ambalo ni la kumlinda mtoto wa kike.
Maembe
amesema tuzo hii itatoa hamasa kwa wengine na itakuwa kielelezo cha
serikali Katika jitihada za kutekeleza tamko la CEDAW linalolenga
kumlinda mwanamke na mtoto wa kike.
Mmoja
wa wafanyakazi wa Chama cha wanahabari wanawake Tanzania TAMWA
akiwakilisha zawadi ya ua kwa Mkurugenzi wao Valerie Msoka baada ya
kukabidhiwa tunzo ya umahiri na utambuzi wa kupinga ndoa za utotoni na
Ukeketaji nchini Tanzania kutoka nchini Canada.
Amesema
serikali itaendeleza jitihada hizo kwa kuhakikisha watoto wa kike
hawaolewi katika umri mdogo kwa kulazimishwa kwa kujenga mazingira
mazuri shuleni yatakayovutia watoto wa kike kubaki mashuleni, kuongeza
hamasa za uelewa wa tatizo na kuhakikisha wale wote wanaohusika na
kuwalazimisha watoto wa kike kuolewa Katika umri mdogo wanachukuliwa
hatua za kisheria. Lakini pia kuharakisha kubadilisha sharia ya Ndoa ya
mwaka 1971 ambayo haimlindi mtoto wa kike chini ya umri wa miaka 18
kuolewa.
“Watoto
2 kati ya 5 hujikuta wako Katika mazingira ya kuozeshwa kwa nguvu
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kutokuwa na elimu ya kutosha,
maisha duni vijijini, umaskini na mila na desturi potofu zinazoendelezwa
na baadhi ya makabila na mahari”, amesema Maembe.
Tafiti
zinaonyesha kwamba asilimia 39 ya watoto wa kike wenye elimu ya msingi
wameolewa katika umri usiotarajiwa chini ya miaka 18 wakati wale wenye
elimu ya kutosha wa mjini wameolewa baada ya kufikisha miaka 18.
Mkurugenzi wa mtendaji wa TAMWA akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Chama hicho.
Ndoa
za utotoni ni pale mtoto wa kike anapoozeshwa kwa lazima akiwa katika
umri chini ya miaka 18 na wakati mwingine yuko shuleni. Madhara yake ni
makubwa kwa afya ya mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na kupoteza uhai wake
na mtoto mwenzake, kukosa maendeleo kimaisha na kuendeleza utamaduni wa
kuwa tegemezi na kudumaza fikra na kumfanya kuwa duni Katika taifa.
Katiba
ya nchi inamlinda mtoto wa kike kwa kutambua kwamba mtoto ni yule
ambaye huko chini ya miaka 18 na hana sifa za kupiga kura. Lakini wakati
huo huo Sheria ya Ndoa 1971 inasema mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka
16 anaweza kuoa na msichana mwenye miaka 14 anaweza kuolewa kwa ridhaa
ya wazazi.
Sheria
hizi mbili zinakinzana na hivyo hazimlindi mtoto wa kike moja kwa moja.
“Tutahakikisha kwamba sheria ya ndoa inafanyiwa marekebisho ili iende
pamoja na Katiba ya nchi, jitihada zinaendelea kwa kuungana na
wanaharakati wote nchini kuleta mabadiliko hasa baada ya kuzindua
kampeni ya “Ukanda Huru wa Ndoa za Utotoni” (Child Marriage Free Zone)
na Graca Machel.
Tuzo
ya CEFM Champion ilishuhudiwa na wadau mbalimbali kutoka serikalini na
mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa kuchangia maendeleo, Umoja wa
Kimataifa, waandishi wa habari na wanajamii.
No comments:
Post a Comment