Halmashauri zitakazonufaika na
malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya
Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014.
Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni
zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya
Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement – MDA) baina
ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara
kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya
Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya
Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali
Mha. Ngosi C.X. Mwihava
KAIMU KATIBU MKUU
25 Februari, 2015
No comments:
Post a Comment