TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, June 10, 2016
SERIKALI: MFUMO WA MALIPO YA UZEENI UPO MBIONI KUANZA
Wazee wakifuatilia hotuba ya Waziri
Ramadhani Juma, OFISI YA MKURUGENZI DODOMA
SERIKALI imesema mchakato wa kuwaingiza wazee wote wasio katika ajira rasmi hapa nchini kwenye mfumo wa malipo ya uzeeni uko katika hatua za mwisho na kwamba wakati wowote kundi hilo litaanza kunufaika na mpango huo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akizungumza na wazee mkoani Dododma alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa asasi zinazojishughulisha na wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya Mkoa wa Dodoma juzi.
Alisema wazee wasio katika ajira rasmi wamefanya mambo makubwa katika maendeleo ya nchi kwa muda mrefu sasa hivyo sio sahihi kuachwa nje mfumo wa pensheni ya uzeeni na kwamba sasa ni wakati muafaka kutambua uwepo wao na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.
Amebainisha kuwa, Serikali ya awamu ya tano chini ya Mh. Rais Dkt. John Magufuli haitashindwa kuwahudumia wazee wa nchi hii ambao idadi yao kwa sasa inakadiriwa kuwa milioni 2.5 na kwamba hilo ni kundi kubwa ambalo halipaswi kutengwa.
Waziri Ummy Mwalimu pia ametoa agizo kwa Halmashauri zote nchini kutenga vyumba maalum kwa ajili ya kuwapatia huduma za afya wazee na kuondokana na dhana ya ‘dirisha la wazee’ huku akiimwagia sifa Halmashauri ya Wilaya Magu Mkoani Mwanza kwa kuonesha mfano huo na kwamba wilaya nyingine ziige hatua hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri huyo ametoa wito kwa taasisi za fedha nchini kuwaamini na kutoa mikopo kwa wazee badala ya kuwaona kama kundi lisiloweza kuzalisha kwani mzee anaweza kufanya shughuli za kuichumi hata akiwa na umri wa miaka 75 hadi 80.
“Wazee wengi wameendelea na shughuli za kuzalisha mali hadi wanafikia umri wa 75 hadi 80 hivyo mabenki yasiwatenge wazee katika kuwawezesha kimitaji ili waendelee na uzalishaji” alisema
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akifuatilia neno la ukaribisho alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Asasi zinazojishughulisha na Wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya mkoa wa Dodoma juzi.
Baadhi ya wazee wa Mkoa wa Dodoma wakijitambulisha kwa Waziri wakati wa Mkutano huo.
Msoma risala ya wazee wote wa Tanzania Bi Clotrida Kokupima kutoka wilaya Kasulu Mkoani Kigoma akisoma risala hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akitoa hotuba yake alipofungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Asasi zinazojishughulisha na Wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya mkoa wa Dodoma juzi.
Baadhi ya wazee wakiwa katika mkutano huo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Dkt. Tom Mtoi mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Mtandao wa Asasi zinazojishughulisha na Wazee Tanzania katika ukumbi wa Maktaba Kuu ya mkoa wa Dodoma juzi.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment