Waziri Mkuu, Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa akimpongeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mpango
mara baada ya kuwasilisha hotuba ya taaarifa ya hali ya uchumi 2015 na mpango
wa maendeleo wa taifa 2016/17 mjini Dodoma .
Serikali
imetenga kiasi cha Tsh. Bilioni 11,820.503 kwa ajili ya kutekeleza
miradi ya maendeleo kwa mwaka wa Fedha 2016/17.Hayo yamesemwa leo
Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Philip Mpango
wakati akitoa hotuba kuhusu taarifa ya hali ya uchumi nchini na mpango
wa maendeleo wa taifa 2016/17.
Waziri
Mpango amesema kuwa kiwango hicho ni sawa na asilimia 40 ya bajeti yote
ya serikali na kuongeza kuwa fedha za ndani ni shilingi bilioni
8,702.697 ambazo ni sawa na asiliia 74 ya bajeti ya maendeleo na fedha
za nje ni shilingi bilioni 3,117.805 sawa na aslimia 26 ya
maendeleo.Aidha, Mpango amesema kuwa sekta binafsi inatarajiwa kuwekeza
kiwango kikubwa cha fedha ili kuanzisha na kuendeleza viwanda ikiwa ni
sehemu ya utekelezaji wa Mpango huo.
“ Kwa
ujumla fedha za maendeleo zimeelekezwa zaidi katika miradi inayolenga
kuendeleza viwanda kama vile uchukuzi,ujenzi, nishati, kilimo, maji,
elimu na afya,”amesema Waziri Mpango.
Ameongeza
kuwa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 umeainisha miradi
mikubwa ya kielelezo ambayo itapewa msisitizo katika utekelezaji wake.
Waziri
Mpango ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa makaa ya mawe ya
Mchuchuma, mradi wa chuma Liganga, ujenzi wa reli mpya kati ya Dar –
Kigoma na Tabora- Mwanza na matawi yake Isaka- Kigali/Keza- Msongati na
Kaliua- Mpanda kwa kiwango cha standard gauge.
Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2016/17 utategemea zaidi ushiriki wa sekta binafsi
No comments:
Post a Comment