Sehemu
ya barabara iliyopo kijijini Matale, Pemba iliyojengwa na Programu ya
MIVARF kwa kiwango cha changarawe ambayo wakulima wa mazao ya ndizi
wanatumia kusafirisha mazao yao kuelekea eneo la soko.
Na. Mwandishi Maalum.Serikali kupitia Ofisi ya waziri Mkuu chini ya Programu ya uboreshajiwa miundombinu ya masoko, uongezaji thamani mazao na huduma za kifedha vijijini (MIVARF) imefanikiwa kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumiendelevu kwa kuziwezesha kaya 63, 562 za Ungunja na Pemba kunufaikamiundombinu ya masoko kwa kukarabati na kujenga barabara za vijijinizinazotoka mashambani na kuelekea eneo la masoko.Programu hiyo katika kuboresha miundo mbinu ya masoko Zanzibar,imeweza kujenga barabara kwa kiwango cha changarawe zenye urefu waKm. 149.5, ikiwa Km. 69.1 kwa upande wa Unguja na Km. 80.4 kwa upandewa Pemba.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam tarehe 09Juni, 2016, Mratibu Mradi huo Taifa, Bw. Walter Swai amesema malengoya mradi ni kufanikisha azma ya Serikali ya kupunguza umaskini nakuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi endelevu kwa kuziwesha kaya zavijijini kujiongeza kipato na usalama wa chakula. Uboreshaji wa miundombinu ya masoko, umeweza kuongeza thamani mazao ya kilimo, nakuwajengea wananchi waishio vijijini uwezo wa kuyafikia masoko.“Miundo mbinu ya barabara iliyojengwa visiwani Zanzibar imewasaidiawakulima kupata barabara za uhakika ambazo zinapitika kwa msimu wotelakini pia uwepo wa barabara hizo umewasaidia wakulima kupunguza muda wa kusafirirsha mazao toka shambani hadi sokoni” alisema Swai.Naye mratibu wa Programu hiyo Zanzibar, Khalfan Salim, alifafanua kuwaProgramu itahakikisha kuwa inafanikisha malengo yake kwa kuboreshamiundo mbinu ya masoko, kuongeza thamani mazao ya kilimo kwa ujenzi wa maghala ya kuhifadhi mazao yao kwa lengo la kuongeza mnyororo wathamani wa mazao.“Programu ya MIVARF inaendelea kutekeleza uboreshaji wa miundo mbinuya masoko hapa zanzibar kwa kujenga masoko na maghala yenye mahitajimaalum kwa kuwa yatakuwa na vyumba maalum vya vipozeo kwa mazao ya matunda na mbogamboga katika hatua za mwisho” alisisitiza SalimKwa nyakati tofauti baadhi ya wakulima wa visiwani Pemba na Ungujawanaojishughulisha na kilimo cha ndimu, mananasi , ndizi na mbogambogawalibainisha kuwa kabla ya ujenzi wa barabara walikuwa wanasafiriishamazao hayo kwa saa moja kutoka shambani hadi sokoni lakini kwa sasawanasafirisha mazao yao kwa muda wa dakika nne kufika eneo la soko.Mkulima wa ndizi kijijini Matale, Pemba, Said Ramadhani alifafanuakuwa ujenzi wa miundo mbinu ya barabara umesaidia thamani ya mazao yao kuongezeka kwa kuwa wanao uwezo wa kusafirisha mazao yao kwa usalama hivyo kuweza kuyafikisha mazao yao sokoni kwa usalama na kwa haraka bila kuharibika na kuptea shambani.Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini(MIVARF) ni Programu ya miaka saba ambayo utekelezaji wake umeanzarasmi mwaka 2011. Programu hiyo inagharamiwa na serikali ya Tanzaniaikishirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) naBenki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB chini ya uratibu wa Ofisi yaWaziri Mkuu
No comments:
Post a Comment