RC MWANZA AKABIDHI VISIWA KWA MALIASILI.
RC MWANZA AKABIDHI VISIWA KWA
MALIASILI. Na Atley Kuni- RS Mwanza. Mkuu wa mkoa wa Mwanza John
Mongella, ameiagiza taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi kuanza
kutumia visiwa na majabali makubwa yaliopo mkoani humo kwaajili ya
mazoezi ili kuweza kusaidia kupambambana na uhalifu ulioanza kujitokeza
katika siku za karibuni katika mkoa huo. Akizungumza katika uzinduzi wa
maonesho ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo
hicho nchini Tanzania, Mongella amesema badala ya wakurufunzi hao
kwenda kufanya mazoezi kwenye maeneo ya nje ya mkoa ni vema kuanzia sasa
mkaanza kutumia visiwa vyetu, “Ndani ya ziwa viktoria, hasa huko
visiwani kuna watu wanafanya uvuvi haramu sasa ni vema wakati wa mazoezi
mkawa mnafanyia kwenye maeneo hao ambayo yamekithiri kwa uvuvi usio na
tija”, alisema Mongella na kuongeza, “lakini sio kukomesha tuu, uvuvi
haramu bali pia itachagiza kwenye suala zima la utunzaji wa mazingira na
maliasili” Amesema kuwa, endapo taasisi hiyo ikitumia sehemu ya mafunzo
kwa vitendo, kama mkoa utakuwa hauna haja yakufunga shughuli za uvuvi
kwa msimu na badala yake itasaidia kwenye uzazi salama wa samaki na
viumbe wengine wa majini. Kwa upande wake mkuu wa chuo hicho bi Lowael
Damalu, amemuelezea mkuu wa mkoa kuwa chuo hicho hivi sasa, kinauwezo
wakudahili wakurufunzi 415 kwa msimu mmoja, ambalo ni ongezeko kubwa
ikilinganishwa na wakurufunzi 50, waliokuwa wakidahiliwa na chuo hicho
wakati kinaanza mwaka 1966, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni
pamoja na kupata ithibati ya kutoka baraza la Elimu ya ufundi, ongezeko
la kozi za askari kuwa (basic technician, Law Enforcement, uboreshaji wa
maslahi ya watumishi, mafanikio mengine ameyataja kuwa ni kuongezeka
kwa miundombinu na vifaa vya kufundishia, lakini pia taasisi kuwa na
tovuti yake ya www.pasiansiwildlife.ac.tz sambamba na taasisi kujipatia
ardhi. Mkuu huyo wa chuo amesema mbali yakuwa na mafanikio chuo hicho
bado kinakabiliwa na matatizo ya uchakavu wa baadhi ya mabweni, uchache
wa nyumba za watumishi, vilevila kutokuwepo kwa sheria ya uanzishwaji wa
taasisi sambamba na uhaba wa ajira kwa wakurufunzi wanao hitimu katika
chuo hicho
No comments:
Post a Comment