TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Friday, June 10, 2016
Halmashauri ya Mji wa Kibaha yakamilisha miradi mitano ya maji
Na Lilian Lundo
Halmashauri ya Mji wa Kibaha imeeleza kuwa upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa mji huo kwa sasa ni asilimia 56 kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.
Akiongea kwa njia ya simu Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Bw. Innocent Byarugaba amesema kuwa Halmashauri ina jumla ya miradi 11 ya maji ambayo mitano imekamilika na sita iliyobaki iko katika hatua za mwisho.
“Maji safi na salama yanapatikana kwa asilimia 56 ikiwa ni juhudi za Halmashauri za kukabiliana na tatizo la maji na mpaka sasa miradi mitano imekamilika ambayo hutoa huduma ya maji kwa wananchi,” alisema Bw. Byarugaba.
Katika kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji unakuwa bora zaidi, Byarugaba amesema kuwa jitihada za kukamilisha upatikanaji wa maji unafikia asilimia 100 ambapo wanaendelea kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa na Halmashauri hiyo.
Aliongeza kwa kutaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na Mradi wa maji Mtaa wa kwa mfipa Galagaza kata ya Msangani, Vikawe kata ya Pangani, Sagale kata ya Viziwaziwa, Zojosa kata ya Misugusugu na Mwanalugali kata ya Tumbi.
Aidha alianisha miradi mingine ya maji inayotegemewa kukamilika kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuwa ni mtaa wa Sofu kata ya Sofu, Muheza kata ya Mailimoja, Kibenge kata ya Msangani, Kibugalo kata ya Visiga, Kalabaka kata ya Misugusugu na Mikongeni kata ya Viziwaziwa.
Bw. Byarugaba alitoawito kwa kuwataka wananchi kuwafichua watu wanaokata mabomba ya maji nakujiunganishia maji kinyemela kwani kwa kufanya hivyo kunapunguza kasi ya majina kusababisha watu wengine kukosa maji.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment