Watanzania waombwa kushiriki siku ya Mtoto wa Afrika.
“Tarehe 16 Juni ya kila mwaka, ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika, katika siku hii, Tanzania inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Afrika kuadhimisha siku hii kwa mujibu wa Azimio lililopitishwa na nchi 51 za Umoja huo mwaka 1990,” imefafanua taarifa hiyo.Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Azimio hilo lilipitishwa kwa ajili ya kukumbuka mauaji ya watoto wa shule yaliyofanyika katika kitongoji cha Soweto, Afrika ya Kusini Juni 16, 1976, ambapo watoto wapatao 2,000 waliuawa kikatili na Makaburu wakiwa katika harakati za kutetea haki zao za msingi za kutobaguliwa kutokana na rangi yao.Katika siku hiyo watoto hupata nafasi maalum ya kujieleza, kusikilizwa, kushirikina kuonyesha vipaji vyao mbele ya wazazi, walezi na jamii kwa ujumla. Watoto wanahaki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa, kushiriki na kutobaguliwa Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “Ubakaji na Ulawiti kwa Watoto Vinaepukika: Chukua Hatua Kumlinda Mtoto.”
No comments:
Post a Comment