TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, June 8, 2016
SERIKALI KUAJIRI WALIMU 35411 KATIKA MWAKA WA FEDHA 2016/17
Jonas Kamaleki-MAELEZO
Serikali katika mwaka wa fedha 2016/2017 inatarajia kuajiri walimu 35,411 katika shule za msingi na sekondari ili kuongeza tija katika sekta ya elimu nchini.
Hatua hiyo ni mkakati wa Serikali wa kukabiliana na upungufu wa walimu 22,460 wa masomo ya Sayansi na Hisabati katika shule za sekondari, hatua inayoelezwa kuwafanya wanafunzi kutofanya vizuri katika masomo hayo.
Hayo yamesemwa jana Bungeni na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Buyugu Kasuku Samson Bilago aliyetaka kujua idadi ya walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati wanaohitajika ili kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014.
Profesa Ndalichako ameongeza kuwa idadi ya walimu wa sekondari waliopo kwa sasa ni 88, 999 kati ya hao walimu 18, 545 ni wa masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo 70, 454 ni wa masomo ya Lugha, Sanaa na Biashara.
Kuhusu uboreshaji wa miundombinu mashuleni Profesa Ndalichako amesema Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji imeendelea kutenga fedha katika bajeti ya kila mwaka kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu mashuleni, ujenzi wa nyumba za walimu, vyoo vya walimu na wanafunzi na ujenzi wa madarasa.
Aidha, Profesa Ndalichako amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 serikali ilitenga bilioni 67.83 ambazo zimeshapokelewa katika Halmashauri mbali mbali na zimetumika kwa ajili ya ukarabati, ujenzi na umaliziaji wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa vyoo na uwekaji wa umeme katika shule za sekondari 528 nchini.
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment