TAN
Bayport
Kikoa
Myway entertainment
FORE PLAN CLINIC
MPINGA CUP 2016
Mashujaa Fm 89.3, Lindi
Wednesday, June 8, 2016
KUKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAZWA KUHUSU MAOMBI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA MWAKA 2016/2017
TAARIFA KWA UMMA
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa zinazosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa imetangaza sifa na vigezo vitakavyotumika katika uchambuzi wa maombi ya mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Taarifa hizo zinazosambazwa, pamoja na mambo mengine, zinaeleza kuwa sifa zitakazotumika kuwa ni ufaulu wa waombaji katika mitihani yao ya elimu ya sekondari na diploma. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa maelezo rasmi yanapatikana katika tovuti ya Bodi ya Mikopo na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Bodi inapenda kuwataarifu wadau wake wote, wakiwemo wale wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya juu kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwaomba wawe na subira wakati Bodi inakamilisha taratibu za uombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017.
Baada ya kukamilika kwa taratibu hizo, mwongozo wa utoaji mikopo utatolewa rasmi na kutangazwa kwa umma kupitia njia mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari na tovuti ya Bodi ya Mikopo (
www.heslb.go.tz
).
IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI,
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU,
JUMANNE, JUNI 7, 2016
Taarifa hii pia inapatikana katika tovuti
ya Bodi (
www.heslb.go.tz
)
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment