Mratibu
wa Kitaifa wa Uzazi Salama, Dr Koheleth Winani ( kulia) na Meneja
Huduma za Jamii Airtel, Hawa Bayumi (katikati) pamoja na Mkurugenzi
Msaidizi Mkazi wa Center for Disease Control (CDC) Tanzania, Dr Maestro
Evans wakipongezana baada ya kuzindua namba maalumu itakayowawezesha
watoa huduma za afya kuwasajili kina mama wajawazito na wenye watoto
kwenye huduma itakayowapa taarifa mbalimbali za afya bure ijulikanayo
kama “Wazazi Nipende”. mradi wenye lengo la kupunguza idadi ya vifo vya
kina mama wajawazito na watoto.
Akiongea
kuhusu ushirikiano huo , Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Bi Hawa
Bayumi alisema” Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu wa wazazi
nipendeni kupitia huduma yetu ya ujumbe mfupi. Mpango huu unaonyesha
uwezo wa teknologia katika jamii na kwamba teknologia ya simu za mkononi
inaweza kutoa mchango mkubwa katika kuokoa maisha ya maelfu ya akina
mama.
Maelfu ya wajawazito, wazazi na wasaidizi wamenufaika na huduma hii. Kwa kutoa huduma hii bure mpaka sasa tumeweza kuwekeza kiasi cha shilingi 1,518, 000,000 na tunaendelea kushirikiana na mhealth Tanzania PP katika kuhakikisha mpango huu unakuwa endelevu na kuwanufaisha watanzania wengi. Airtel tumejipanga kuendelea kuhamasisha usalama katika maisha ya watanzania na kuwawezesha jamii kufatilia na kutia mkazo katika afya zao kwa kuwapatia elimu juu ya afya bure bila gharama zozote.”

No comments:
Post a Comment