Mwanamuziki
Nyota wa Kike nchini Judith Wambura a.k.a Lady Jay Dee anayetamba na
kibao chake cha #NdiNdiNdi amefanya onyesho alilolipa jina la
#NaamkaTenaTour katika viwanja vya Royal Village, onyesho
lililohudhuriwa na watu na watu mbalimbali akiwemo Naibu Spika wa Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Waheshimiwa
Wabunge, Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez pamoja
mashabiki wake mkoani Dodoma.
Mh. Halima Mdee akipata Ukodak na wananchi wa Dodoma wanaomkubali.
Mh. Halima Mdee akipata Ukodak na wananchi wa Dodoma wanaomkubali.
Mwanamuziki Lady Jay Dee na The Band wakitoa burudani kwa wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake katika harakati za kuwafikia mashabiki wake wote nchini nzima kwa show aliyoi' brand' kama Naamka Tena Tour.
Vijana watanashati wa bendi Lady Jay Dee wakitoa burudani kwa mashabiki wa Dodoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kwenye viwanja vya Royal Village ilipofanyika show ya mwanamuziki Lady Jay Dee mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez (kulia) akiteta jambo na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mh. Shyrose Bhanji kwenye show ya Lady Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma.
Mh. Esther Bulaya akiserebuka na Hoyce Temu katika show ya Lady Jay Dee iliyofanyika mwishoni mwa juma mjini Dodoma.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Kawe, Mh. Halima Mdee walipokutana kwenye show ya Lady Jay Dee.
Upendo waliounyesha watu wa Dodoma kwa mwanamuziki Lady Jay Dee.
No comments:
Post a Comment