JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
WIZARA
YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
|
|
|
Simu: +255-22-2112035/40
|
S.L.P. 9223
|
|
Nukushi: +255-2122617/2120486
Barua pepe:ps@moha.go.tz
|
Dar es Salaam
|
|
|
Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara yake ya Uhamiaji imewahamisha
jumla ya Maofisa na askari wa Idara ya Uhamiaji hamsini na tisa (59)
kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake walikokuwa
wakifanya kazi na kupelekwa sehemu mbalimbali nchini.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest
Rwegasira amesema uhamisho huo umefanyika ili kuongeza ufanisi wa
utendaji kazi katika Idara ya Uhamiaji.
Kwa
mujibu wa Jenerali Rwegasira zoezi hilo la kuwahamisha Maofisa wa Idara
ya Uhamiaji linaendelea kufanyika nchi nzima ikiwa ni hatua za
kuboresha utendaji kazi na hivyo kuongeza ufanisi zaidi wa kiutendaji.
Jenerali
Rwegasira ameeleza kuwa watumishi wote waliopewa uhamisho wanatakiwa
kuripoti kwenye vituo vyao vipya mara moja na kutoa angalizo kuwa
mtumishi yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa visingizio mbalimbali
atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kuachishwa kazi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
5 Juni, 2016
No comments:
Post a Comment