Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi.
Na Mwanadishi Wetu
Mshindi
wa Januari 2015 wa shindano la wazo la biashara 3N alitarajiwa
kutangazwa siku ya leo Alhamisi ya Februari 12 kuanzia saa tano asubuhi
jijini Dar es salaam.
Kwa
mujibu wa Dk. Reginald Mengi kupitia kurasa wake wa twitter, alitangazia
umma kuwa Shindano hilo jipya lijulikanalo kwa kifupi -3N, ikiwa ni
kifupisho cha ‘Nitabuni wazo la biashara, Nitatekeleza, na
Nitafanikiwa’, ambapo mshindi wa kwanza wa mwezi Januari alitarajiwa
kutangazwa siku ya leo ya alhamisi Februari 12.
Dk.
Mengi aliweka ujumbe huo twittter : “Kutokana na sababu zisizozuilika
mshindi wa Januari wa shindano la 3N atatangazwa Februari 12 saa 5
asubuhi. Samahani kwa usumbufu wowote”.
Kwa
mujibu wa Dk. Mengi awali mshind I alitakiwa kutangazwa Jumatano ya jana
ya Februari 11, kabla ya kusogeza mbele hiyo Februari 12.
Shindano
hilo litakuwa linafanyika kila mwezi kwa muda wa miezi sita kuanzia
Januari Mosi 2015, hadi Juni 30, 2015, na mshindi wa kila mwezi
atajishindia ruzuku ya shilingi milioni 10 atakazozitumia kutekeleza kwa
vitendo wazo lake la biashara.
Shindano
hilo, linawashirikisha Watanzania pekee, litaendeshwa kwa njia ya
mtandao wa kompyuta ambapo mshiriki atatuma wazo lake la biashara kwa
anuani ya twita @regmengi Shindano
la Wazo la Biashara. Katika mchujo wa kwanza jopo la wataalamu litateua
mawazo 10 bora Zaidi na waliotoa mawazo hayo watafanyiwa usaili kwa njia
ya simu ili jopo hilo lijiridhishe kama mawazo waliyoyotuma ni yao
binafsi, na kama wamejipanga vizuri kutekeleza kibiashara.
Kutokana
na mawazo hayo 10 teule, jopo litachagua wazo moja kuwa mshindi. Hii ni
mara ya tatu kwa Dkt. Mengi kuendesha shindano kwa kutumia mtandao wa
kompyuta wa twitter kwa kuamini kwake kuwa mitandao ya kijamii ina nguvu
kubwa katika kuchochea ujasiriamali hasa kwa kizazi cha sasa.
Shindano
la kwanza na la pili lililoendeshwa mwaka jana lilikusudiwa kushawishi
mawazo ya kuondoa umaskini katika taifa lenye utajiri mkubwa, lakini
watu wake wengi wakiwa bado wametopea katika lindi la umaskini.
Awali
akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo, Dkt. Mengi alisema
shindano hilo limelenga kuhimiza watu kuwa na upeo mkubwa wa kuona fursa
za kibiashara na kuzitumia kujikwamua kiuchumi. Pia alisema shindano
hilo ni mchango wake binafsi wa kuunga mkono jitihada za serikali na
sekta binafsi za kuwakomboa wananchi kiuchumi kwa njia za ujasirimali,
kwani amesema Sera zote mbili za kitaifa za Elimu ya juu na maendeleo ya
viwanda vya kati na vidogo zina vipengele vya kuchochea na kuendeleza
utamaduni wa ujasirimali wa mtu mmoja mmoja.
“Kwa
muda mrefu nimekuwa nikishawishi uwepo wa moyo wa ujasirimali miongoni
mwa wa Watanzania na hasa kwa vijana. Ni ndoto yangu kuona uchumi wetu
unakua kwa kasi kiasi cha kuzalisha zaidi ya mamilionea 100 kila mwaka
wanaoendesha biashara halali,” alisema.
Alisema kuwa na wazo sahihi la biashara, katika muda muafaka na eneo sahihi ni muhimu zaidi kuliko ruzuku ya fedha.
“Nataka
vijana watambue kwamba wanaweza kuanza na kitu kidogo na kukua kufikia
kampuni kubwa kabisa ya kimataifa unayoweza kufikiria,” alisema na
kusisitiza kwamba anaamini siku moja mazingira ya ujasirimali nchini
Tanzania yakuwa miongoni mwa mazingira bora kabisa barani Afrika.
Amesisitiza
kuwa Shindano hilo liko wazi kwa watanzania wote na wanachotakiwa
kufanya ni kuhakikisha wanapeleka wazo lao la biashara kwa Dk Mengi
kupitia mtandao wa kompyuta wa twita, kwa kumtag Dk Mengi kwenye @regmengi.
Aidha
amesema ni wale tu watakaomtag ndio watafikiriwa na jopo la wataalamu,
na kusisitiza kuwa maamuzi ya jopo la Wataalamu yatakuwa ni ya mwisho.
Washindi
wa kila mwezi wataarifiwa kwa kutumiwa ujumbe mfupi kwa kupitia akaunti
zao za twita (DM) na kupewa ruzuku yao katika sherehe fupi
itakayohudhuriwa na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment