JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MHAMIAJI HARAMU MMOJA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MEKESA ABADA (27) KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI
BILA KIBALI. AIDHA MHAMIAJI HUYO ALIKUWA PAMOJA NA MWENYEJI WAKE AITWAYE
ADIKO MICHAEL (32) MKAZI WA MWANJELWA AMBAYE NAE AMEKAMATWA.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 11.02.2015 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO
KATIKA ENEO LA BARABARA YA SITA, SOKOMATOLA, KATA NA TARAFA YA SISIMBA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA
MAKONGOLOSI WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA JUMA (18)
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI MSOKOTO
MMOJA SAWA NA UZITO WA GRAM 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE
11.02.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA
MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA BAADA YA
KUFANYIKA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA VITENDO VYA KUSHIRIKI KUWAINGIA RAIA WA KIGENI NCHINI BILA
KUFUATA TARATIBU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWAO. AIDHA
ANATOA WITO KWA JAMII/VIJANA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment