a
Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemfungia mechi
tatu beki George Michael Osei wa Ruvu Shooting kutokana na makosa ya
kinidhamu aliyoyafanya akiwa uwanjani.
Osei ambaye alilalamikiwa na TFF
kwa kumkaba na kumchezea kibabe mshambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe
ambapo ni kinyume na mchezo wa kiungwana (fair play) ameadhibiwa kwa
kuzingatia Ibara ya 48(1)(d) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012.
Mlalamikiwa alifika mbele ya
Kamati hiyo jana (Februari 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso
alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji
Maguri kwa kitendo hicho.
Akisoma uamuzi huo, Makamu
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema Osei alipopewa
nafasi ya kujitetea alikana kufanya kosa hilo na kudai magazeti
yametengeneza picha hizo. TFF iliwasilisha ushahidi wa magazeti mawili
ya Championi na moja la The Guardian kwa kuzingatia Ibara ya 96(3) ya
Kanuni ya Nidhamu ya TFF Toleo la 2012.
Katika uamuzi wake, Kamati imesema
kitendo cha Osei ni kinyume na kanuni ya mchezo wa kiungwana (fair
play), na kuongeza kuwa kanuni za TFF kwa makosa kama hayo ni dhaifu,
hivyo kuagiza zirekebishwe ili ziweze kuwa kali zaidi.
Katika hatua nyingine Kamati hiyo,
imetupa malalamiko yaliyowasilishwa na TFF dhidi Katibu Mkuu wa Chama
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM), Mugisha Galibona, na Katibu wa
Simiyu (SIFA), Emmanuel Sorogo.
Kwa upande wa Sorogo, Kamati
imesema baada ya kupitia vielelezo vya pande zote, hasa upande
mlalamikiwa imeridhika kuwa hakushiriki katika kumpiga refa kwenye mechi
ya Kombe la Taifa kwa Wanawake kati ya Shinyanga na Simiyu.
Badala yake aliyehusika ni Kocha
wa Simiyu, Emmanuel Babu ambaye tayari uongozi umeshachukua hatua dhidi
yake kwa kumsimamisha kwanza wakati akisubiri kufikishwa mbele ya Kamati
ya Nidhamu ya SIFA.
Pia barua ya kumsimamisha kocha
huyo ilitumwa kwa Katibu Mkuu wa TFF na Mkurugenzi wa Mashindano. Kamati
imeyachukulia maneno ya mlalamikiwa kuwa ni sahihi ndiyo maana
hayakupingwa na TFF, hivyo malalamiko dhidi ya mlalamikiwa hayana msingi
na yametupwa.
Kwa upande wa Galibona ambaye
ripoti za Kamishna na refa zilionyesha kuwa alishiriki kuhamasisha
marefa kupigwa baada ya mechi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya
Polisi Mara FC na Mwadui FC, Kamati imesema mlalamikiwa aliwasilisha
vielelezo vinne kuthibitisha kuwa hakuhusika.
Kamati imesema licha ya ripoti ya
Saleh Mang’ola kumtaja Galibona, lakini maelezo ya refa huyo na msaidizi
wake Rebecca Mulokozi waliyoandika Kituo cha Polisi baada ya tukio hilo
hayakumtaja mlalamikiwa mahali popote.
Pia barua ya FAM kwenda TFF kuhusu
matukio ya mechi hiyo yanamtoa hatiani mlalamikiwa, hivyo Kamati
imeamuru kuwa malalamiko dhidi ya Galibona hayana msingi na yametupiliwa
mbali.
No comments:
Post a Comment