Jaji
Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga Jaji Kakusulo Sambo akisoma
hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo mapema leo tarehe 12 Februari 2015.
Mafunzo hayo ya siku mbili yanayoshirikisha Mikoa ya Rukwa na Katavi
yanafanyika Mkoani Rukwa. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella
Manyanya na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi.
Jaji
wa Mhakama Kuu ambae pia ni Mkuu wa Chuo cha Mahakama Lushoto Jaji
Ferdinand Wambali akiendesha mafunzo hayo ambayo yameanza leo tarehe 12
Februari na yatamalizika kesho tarehe 13 Februari 2015 katika ukumbi wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa (RDC).
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi Dkt. Ibrahim Msengi akitoa shukurani za Mikoa ya
Rukwa na Katavi kwa kuletewa mafunzo hayo ambayo ni muhimu kwa Kamati za
maadili za Mikoa hiyo katika utekelezaji wa majukumu yake ya siku.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu
Iddi Kimanta (wa kwanza) na Katibu Tawala Wilaya Kalambo Bi Mapinduzi
Severian ambao ni Wajumbe wa Kamati ya maadili Mkoa wa Rukwa
wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati za maadili Mkoa wa Rukwa na Katavi wakifuatilia mafunzo hayo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa (wa kwanza) na wajumbe
wengine wa Kamati za Maadili Mikoa ya Rukwa na Katavi wakifuatilia
mafunzo hayo.
Mafunzo yakiwa yanaendelea.
Picha ya pamoja.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment