Misri imesimamisha kwa muda usiojulikana ligi kuu ya nchi hiyo baada ya watu zaidi ya Watu 20 kufariki dunia.
Kati
ya waliofariki ni wengi wao ni Mashabiki wa timu ya Zamalek ambao
walifariki kutokana na msongamano wakati Polisi walipowafyatulia mabomu
ya machozi baadhi ya mashabiki waliokuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu
ndani ya uwanja wakati timu hiyo ilipokuwa ikipambana na timu ya ENPPI.
Mtandao
mmoja nchini humo uitwao AL-Misriyun umeripoti.Tukio hilo limetokea
baada ya Polisi kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha mashabiki
walikokuwa wakitumia nguvu kujaribu kuingia uwanjani.
Taarifa ya
Wizara ya mambo ya ndani ya Misri inasema kuwa Mashabiki wa Zamalek
walikuwa wanataka kuingia uwanjani kwa nguvu hivyo walikuwa wakiwazuia
ili kunusuru mali ya uma isiharibike.
Polisi wamesema mashabiki
hao walikuwa wanataka kuingia uwanjani bila tiketi, wamenukuliwa
wakisema Watu hao walipoteza maisha baadhi kutokana na msongamano mkubwa
wengine walipokuwa wakipambana na Polisi.
Ndani ya uwanja kulionekana rundo la viatu karibu na miili ya Watu waliopoteza maisha na wengine waliolala wakiwa majeruhi.
Mashabiki wa Zamalek wanadai kuwa vurumai zilianza mamlaka ya uwanja ilipofungua Geti la waya kuwaruhusu kuingia ndani.
Mashuhuda
wanasema uzio ulianguka wakati Watu walipokuwa wakipigania kuingia
ndani hali iliyosababisha msongamano mkubwa, mara askari wa usalama
walianza kurusha mabomu ya kutoa machozi.
Watu walianza kukanyagana hali iliyosababisha Watu kupoteza maisha.
Tukio
hili limetokea ikiwa ni miaka mitatu tangu Wapenzi wa soka zaidi ya 70
walipopoteza maisha wakati vurugu zilipotokea katika uwanja wa ndege wa
Port Said.
Baada ya tukio hilo idadi maalum iliwekwa kwa
watakaohudhuria Mechi kwa hofu ya hali ya usalama ,inaelezwa kuwa mipaka
hiyo iliyoondolewa hivi karibuni huwenda ikawekwa tena baada ya tukio
la mwishoni mwa juma lililopita.
No comments:
Post a Comment