Mke wa Rais na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Mwalimu Mkuu Ndugu Fadhili Mtitima wa Shule ya Msingi
Mpilipili iliyoko Manispaa ya Lindi tarehe 11.2.2015. Mama Salma
alikwenda shuleni hapo kuwatembelea wanafunzi wenye mahitaji maaalum.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa
ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akimsikiliza mtoto mwenye
mahitaji maalum Mohammed Hashim aliyeweza kuimba vizuri wimbo wa Taifa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpongeza mtoto Mohammed Hashim mara baada ya kuimba wimbo wa Taifa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akishiriki kufundisha darasa la wanafunzi wenye mahitaji maalum
wanaosoma katika Shule ya Msingi Mpilipili huko Lindi tarehe 11.2.2015.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa
ya CCM Mama Salma Kikwete akisahihisha madaftari ya wanafunzi wenye
mahitaji maalum wanaosoma Shule ya Msingi Mpilipili katika Manispaa ya
Lindi mara baada ya kuwafundisha na kuwapa zoezi wanafunzi hao tarehe
11.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
aizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mpilipili mara baada ya
kutembelea kitengo cha elimu maalum shuleni hapo tarehe 11.2.2015.
Mke wa Rais na Mjumbe wa NEC Taifa
ya CCM Mama Salma Kikwete akizungumza na viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi Tawi la Mtuleni B katika Kata ya Matopeni huko Lindi Mjini
tarehe 11.2.2015.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria
mkutano wa hadhara uliofanyika katika Tawi la CCM Mpilipili Kaskazini
wakimsikiliza kwa makini Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani)
wakati alipowahutubia tarehe 11.2.2015.
Mke wa Rais na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete
akiwahutubia mamia ya wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa
hadhara uliofanyika katika Tawi la Mpilipili katika Kata ya Nachingwea
huko Lindi Mjini tarehe 11.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwapungia mamia ya wananchi wa Kata ya Nachingwea baada ya kuhutubia
mkutano wa hadhara kwenye Tawi la Mpilipili Kaskazini huko Lindi Mjini
tarehe 11.2.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment