TAN

TAN

Bayport

Bayport

Kikoa

Kikoa

Myway entertainment

Myway entertainment

FORE PLAN CLINIC

FORE PLAN CLINIC

MPINGA CUP 2016

MPINGA CUP 2016

Mashujaa Fm 89.3, Lindi

Tuesday, February 10, 2015

Airtel yazindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi kwa Wakazi wa Mwaza

Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akiongea na waandishi wa habari ( pichani hawapo) wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku. kushoto Afisa Masoko wa Airtel Rebecca Mauma na Kulia ni Afisa Mauzo kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael.
 Afisa Masoko wa Airtel Rebecca Mauma (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku. katikati ni Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde akifatiwa na Afisa Mauzo kanda ya Ziwa Emmanuel Raphael 
 Wanahabari wa vyombo mbalimbali Jijiji Mwanza wakifatilia utambulisho wa promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijiini Mwanza wakati wa mkutano wa kuzindua na kuitambulisha promosheni hiyo kwa wakazi wa mwanza
 Wanahabari wa kutoka vyombo vya habari Mwanza wajadili kuhusu promosheni ya Airtel yatosha Zaidi wakati wa kuzindua promosheni ya Airtel yatosha Zaidi jijini Mwanza, Promosheni ya Airtel yatosha inawawezesha wateja wa Airtel kujishindia gari Aina ya Toyota IST moja kila siku

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua promosheni ya Airtel Yatosha Zaidi kwa wakazi wa Mwanza wakati ziara yake yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake juu ya promosheni hiyo kambambe inayowawezesha wateja wake kujishindia gari Aina ya Toyota IST kila siku
Promosheni ya Airtel yatosha Zaidi iliyozinduliwa Jumatatu wiki iliyopita mpaka sasa imewawezesha wateja wa 3 kutoka katika mikoa mbalimbali kujishindia magari  aina ya Toyota IST kufatia droo iliyochezeshwa ijumaa iliyopita chini ya usimamizi wa bodi ya mchezo ya kubahatisha Tanzania
Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Tunayofuraha kuitambulisha kwenye wakazi wa mkoa wa Mwanza promosheni yetu ya Airtel Yatosha  Zaidi ninayomuwezesha wateja wetu kuendelea kufurahia vifurushi vya huduma ya Airtel yatosha huko wakijishindia Toyota IST Moja kila siku. 
Mpaka sasa tunao washindi wa tatu ambao wamepatikana kupitia droo iliyochezeshwa siku ya Ijumaa iliyopita, wewe pia unayo nafasi ya kuibuka mshindi kwa kujiunga tu na vifurushi vya Airtel yatosha vya siku, wiki au Mwezi namba yako itaingia moja kwa moja kwenye droo, hakuna makato yoyote wala gharama ya ziada ni kwa matumizi yako yakaawaida ya kila siku tunakuwezesha kushinda zawadi nono.
Akitangaza majina ya washindi Bi Jane Matinde alisema washindi wetu katika droo yetu ya kwanza ni pamoja na Ramadhani Dilunga, Mkulima  Mkazi wa mkoa wa Pwani, Namtapika Kilumba, mwalimu Mstaafu na mkazi wa mkoa wa Mtwara  pamoja na Mwajabu Churian , mfanyabiashara na mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Saalam. Bado kuna magari 57 yamebaki kwa wewe mteja wa Airtel kujishindia
Natoa wito kwa wakazi wa Mwanza na watanzania kwa ujumla kujiunga katika vifurushi hivi kwa kupiga *149*99* au kwa kununua Vocha ya Airtel Yatosha au kwa kupitia huduma ya Airtel Money na kupata vifurushi vya sms, muda wa maongezi na internet zaidi kulinganisha na zifurushi vingine sokoni lakini zaidi Airtel yatosha inakupati nafasi ya kushinda Toyota IST kila siku aliongeza Matinde
Kwa upande wake mkazi wa Mwanza Bwana Selestine Bundala alisema” tumefurahia sana promosheni hii kwani inatupa nafasi ya kujishindia bila kutuma ujumbe mfupi wala kujibu maswali lakiini zaidi inampaita mshindi gari la kisasa na kumwezesha kufanya shughuli zake kirahisi, nawapongeza Airtel sana na mimi pia naendelea kuvitumia vifurushi hivi kwani vinarahisisha huduma za mawasiliano na kuzifanya kuwa za gharama nafuu.
Droo ya pili ya promosheni ya Airtel yatosha zaidi itafanyika ijumaa hii ambapo washindi saba wa wa wiki hii watatangazwa. Na washindi watatu wa wiki iliyopita watabithiwa magari yao siku ya Jumatano.

No comments:

Post a Comment